Pages

Thursday, August 08, 2013

MUSSA HASSAN MGOSI ASAINI MTIBWA SUGAR.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Mussa Hassan Mgosi amejiunga rasmi na klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro.

Mgosi ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia klabu ya JKT Ruvu amejiunga na Mtibwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Akiongea na mtandao huu, kocha wa Mtibwa Sugar  Mecky Mexime amethibitisha kwamba klabu yake imemsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, "Mgosi anakidhi vigezo vya mshambuliaji tunayemhitaji baada ya kuondoka wa Javu aliyejiunga na Yanga. Ameshaini mkataba wa mwaka mmoja na atajiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya hivi karibuni."

FABREGAS AIKATAA RASMI MAN UNITED.


Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas hatimaye amevunja ukimya kuhusu suala la Manchester United kutaka kumsajili kwa kusema anataka kubaki nchini Spain.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Kuala Lumpur mahala ambapo  Barcelona wapo kwa ajili ya maadalizi ya msimu mpya. 

Fabregas alisema: 'Ndoto yangu siku zote imekuwa kuichezea Barcelona na hakuna kilichobadilika. Nina furaha sana kuwa hapa na sijawahi kufikiria kuhusu kuondoka.

"Sijawahi kuwa na shaka juu hilo. Haijanigharimu chochote kurudi Barcelona na sasa nataka kuwa mshindi nikiwa hapa.  

'Ni heshima kubwa kwa Manchester United kuleta ofa mbili kwa ajili yangu, lakini hakujawahi kuwa na mazungumzo. Sijawahi kuongea na klabu yoyote tangu nimejiunga na Barcelona miaka miwili iliyopita.
'Siku zote nimekuwa nikitambua ninavyothaminiwa na klabu. Kila mut ameniambia namna anavyonitegemea, sijwahi kupata ishara yoyote tofauti ya kuhisi sihitajiki.
'Sikutaka kusema lolote huko mwanzo kwa sababu kwangu mimi kila kitu kilikuwa wazi kwamba nilikuwa nataka kuendelea kubaki hapa. Niliiambia klabu nitaongea itakapofika zamu yangu.
'Kuna baadhi ya vitu vilitengenezwa, lakini havikuwa vya kweli - hasa la kusema kwamba nimeomba kuongezewa mkataba,' alisisitiza Cesc Fabregas.

MANJI AITISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA WA WANACHAMA WA YANGA KUJADILI KUHUSU AZAM TV.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

1.   Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu (Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016

2.   Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha kuwamkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGAzisirushwe hewani na Azam Media.

Kwa kuwa wawazi, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA kupitia vyombo vya habari tarehe 29 Julai, 2013 ambapo iliweka bayana sababu zake na kueleza kuwa YANGAhaina tatizo na vilabu vingine vya mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake za Vodacom Premier League katika Azam Television.

3.   Sote tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya ziada” inatumika kupotosha msimamo wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha Klabu ya YANGA hadharani.

Juu ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu ambavyo vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu, havina uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati ya Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu zinazojionyesha wazi.

Inadhihirika wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama kuilazimisha YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.

Kwa kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu.

Kwa kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi waje tujadiliane na kuamua suala la Azam Television kurusha mechi za YANGA.

LUIS SUAREZ: "TULIKUBALIANA NA LIVERPOOL IKIWA TUTASHINDWA KUFUZU CHAMPIONS LEAGUE WATANIUZA".

Luis Suarez ameiambia klabu yake ya Liverpool kuheshimu makubaliano yao ya kumruhusu kuondoka endapo klabu hiyo isingeweza kufuzu kucheza klabu bingwa ya ulaya msimu huu unaokuja.

Mshambuliaji huyu amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu vya Arsenal huku ofa mbili tayari zikiwa zimekataliwa na Liverpool - ikiwemo ya £40m ambayo mshambuliaji huyo anasema ilitenguwa kifungu cha kumruhusu kuuzwa kwenye mkataba wake ambao alisaini miezi 12 iliyopita.

"Mwaka jana nilipata nafasi ya kujiunga na klabu kubwa barani ulaya lakini niliamua kubaki kwa maelewano kwamba ikiwa msimu huu ingeshindikana kufuzu kucheza Champions League basi ningeruhusiwa kuondoka," Suarez ameliambia gazeti la Guardian.

"Nilijitoa kwa yote msimu uliopita lakini haikutosha kutufanya kumaliza kwenye top 4 - sasa ninachokitaka ni Liverpool kuheshimu maelewano yetu."

Suarez pia ameonyesha wazi yupo tayari kuipeleka kesi yake kwa kamati ya Premier League ili kuhakikisha azma yake inafanikiwa.
Aliendelea: "Walinipa ahadi na tuliandika mkataba kuhusu hilo na sasa nipo tayari kulipeleka hili suala Premier League ili wao waamue kesi hii lakini sihitaji suala hili lifikie huko.
"Sidhani kama nimesalitiwa, lakini klabu iliniahidi mwaka mmoja uliopita na mimi nilifanya hivyo kwa kuwaambia kama tutafuzu ikiwa tungepata nafasi ya kushiriki Champions League.

"Walinipa ahadi hiyo mwaka mmoja uliopita na sasa nataka waheshimu ahadi yao. Sio kitu tulichokubaliana kwa mdomo tu bali kiandikwa kwenye mkataba. Siendi kwenye kwenye klabu nyingine ili kuiumiza Liverpool."

Friday, August 02, 2013

KIBADENI AMUITA HUMUDI


Kiungo mkabaji wa zamani Azam FC, Abdulhalim Humoud ameibukia Simba akisaka nafasi ya kusajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Humoud aliyemaliza mkataba wake na Azam FC Mei, mwaka huu na kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa na klabu ya Jomo Cosmos, yuko kambi ya Simba iliyopo, Kigamboni, Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili  jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are alithibitisha mchezaji huyo kuwepo kwenye kambi ya timu yake akisaka nafasi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi,  Agosti 24.
Itang’are alisema kuwa Kocha Abdallah Kibadeni ndiye aliyemtaka mchezaji huyo anayedaiwa kufuzu na klabu ya Jomo Cosmos.
“Kocha ndiye ametaka aje kambini kufanya mazoezi na timu ili aweze kujiridhisha na kiwango chake kabla ya kusaini mkataba,” alisema na kuongeza.
“Kamati ya Usajili Simba, tunasubiri kauli ya mwisho kutoka benchi la ufundi na kufanya naye makubaliano ya kusaini mkataba.”
Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni alisema jana kuwa, yuko kwenye kambi ya Simba kwa siku tano sasa akifanya mazoezi na wachezaji wenzake.
“Maendeleo yake ni mazuri ingawa siwezi kusema lolote kwa sasa. Ni mchezaji ambaye namjua vizuri, siyo mgeni kwangu. Pia najua aliwahi kuichezea Simba kipindi cha nyuma kabla ya Azam FC.” alisema Kibadeni.
Humoud alipofuatwa na gazeti hili baada ya kumaliza mazoezi alisema: “Sitaki kuzungumza lolote kwa sasa, ni mapema.”
Humoud alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar na kutolewa kwa mkopo na klabu hiyo kwenda Azam FC.
Wakati huohuo, mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Hussein Javu amejiunga na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga na jana asubuhi alifanya mazoezi.
Javu aliyekuwa akitolewa macho na Simba, amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili mpaka mwaka 2015.
Kusajiliwa kwake ina maana, Yanga haina tena mpango wa kumsajili mshambuliaji  wa kimataifa kutoka Nigeria, Ogbu Brendan.
Mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka jina lake kuandikwa kwenye gazeti kwa kuwa siyo msemaji, alithibitisha kusajiliwa kwa Javu

UCHAGUZI MKUU WA TFF HATARINI KUFANYIKA TENA

Siku ya leo ndio siku ambayo ilitakiwa fomu za kugombea uchaguzi wa mkuu wa TFF zilipaswa ziwe zimeanza kutolewa lakini mpaka sasa hakujawepo na tangazo lolote kutoka TFF kuhusu uchukuaji fomu kwa wagombea watakaopendelea kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

Mtandao huu ulijaribu kufanya uchunguzi kufuatilia nini tatizo nyuma ya uchelewaji huu wa kuanza mchakato wa uchaguzi, tukaja kugundua kwamba tatizo ni kwamba katiba iliyofanyiwa marekebisho na mkutano mkuu wa TFF hivi karibuni imekataliwa kusajiliwa na msajili wa vyama vya michezo.


Kwa mujibu wa uchunguzi wetu katiba ya TFF imekataliwa kusajiliwa na msajili kutoka na kutokidhi vigezo vilivyowekwa kwa ajili ya katiba kuwa halali kusajiliwa.


Kisheria ili katiba ipate uhalali wa kusajiliwa na msajili inabidi ufanyike utaratibu wa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na baada ya hapo 2/3 ya wajumbe wapitishe mabadikiko ya katiba hiyo ndipo itakapopata uhalali wa kusajiliwa na msajili wa vyama vya michezo.


Kingine kilichokwamisha usajili ni kitendo cha TFF kuteua kamati mbali mbali mpya kabla ya katiba kusajiliwa. Sasa waliteua kamati kwa kutumia uhalali wa kamati gani?

NAGOMBEA UENYEKITI SIMBA

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kuwa anafikiria kugombea uenyekiti wa klabu hiyo katika uchaguzi ujao.
“Kweli mimi si kiongozi wa Simba kwa sasa, lakini ni mwanachama wa Simba na kikatiba nina haki ya kuendelea kuitumikia klabu yangu bila kipangamizi chochote hata kuwa Mwenyekiti wa klabu, haimanishi mimi kujiuzulu ndio mwisho wa kuwa kiongozi katika Simba, katiba hainizuii hivyo naweza kurudi na kuifanyia kitu klabu yangu kama kiongozi.”
Kaburu alisema kujiuzulu kwake kama kiongozi ilitokana na kutaka kupumzika na  kujipanga upya.
 “Watu wasiwe na hofu, ninakuja upya na wakati huu nitaangalia matatizo mbalimbali na kuyasuluhisha ili klabu kama klabu ifanikiwe,”alisema.
“Sasa nimetoka kwenye uongozi, nafikiri bado mimi mwanachama wa Simba naruhusiwa kutoa maoni yangu au hata saa zingine kuisaidia Simba kwenye mambo mbalimbali,” alisema Kaburu, ambaye kuonekana kwake mazoezi katika siku za karibuni kuliibua mjadala kwa mashabiki.

Thursday, August 01, 2013

GONZALO HIGUAIN NA PEPE REINA WALIVYOTAMBULISHWA KUITUMIKIA NAPOLI

Argentine striker striker Gonzalo HiguainArgentine striker striker Gonzalo Higuain



Big money: Higuain was on the verge of joining Arsenal before a £34.5million move to Italy
Argentine striker Gonzalo Higuain
Higuain salutes the Napoli cheering fans

XAVI: "BALE SIO WA THAMANI YA MILLIONI 90 - CESC FABREGAS BADO ANA FURAHA CAMP NOU"

Kiungo huyo wa Hispania amenukuliwa akisema kwamba bado hajamuangalia vizuri nyota huyo wa Spurs kiasi cha kumfanya kutoa maoni yake kuhusu kutakiwa kwake na Real Madrid. 

Alisema: “Sidhani kama Bale ana thamani ya fedha hizo zinazotajwa.
Kiukweli kabisa sijawahi kumuona akicheza dakika 90 zote.

Xavi pia alisisitiza  Cesc Fabregas ana furaha kuwepo ndani ya Barcelona, pamoja na kutakiwa na Manchester United.
Kiungo huyo alisema: “Anaonekana kutulia, ana mkataba hapa. Anajituma mazoezini na anacheza vizuri.
"Kuhusu kuondoka, nadhani ni tetesi tu. Tutaona kitakachotokea lakini kwa sasa anaonekana kutulia na tayari kwa msimu mpya na Barcelona.

SAKATA LA YANGA KUPINGA MECHI ZAO KUONYESHWA AZAM TV WANACHAMA WA KLABU WAUNGA MKONO

Uongozi wa matawi wa klabu ya Yanga (wenyeviti na makatibu) leo umefanya kikao katika makao makuu ya klabu mtaa wa twiga/jangwani kisha kutoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuhusiana na tamko la uongozi (kamati ya utendaji) kutokubali kuonyeshwa kwa michezo yake kwenye luninga.
Awali klabu ya Yanga juzi kupitia kamati ya utendaji ilifanya mkutano na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa klabu kuhusiana na kutoridhishwa na kamati ya muda ya Ligi (TPL) kuingia makubaliano ya kurushwa matangazo ya televsheni kwenye michezo yake.
Akiongea na waandishi wa habari leo katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako alisema baada ya kukaa na viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga jijni Dar es salaam kwa pamoja wamekubali na kuunga mkono hoja zilizowasilisha na viongozi juu ya haki ya matangazo.
Mmoja wa viongozi wa matawi Bakili Makele akiongea kwa niaba ya viongozi wa matawi, alisema TFF inaamua kukandamiza soka la Tanzania kwa kuviamulia maamuzi yake juu ya kuonyeshwa kwa michezo ya timu kwenye luninga.
Makele amesema taratibu za kuipa kampuni ya Azam TV tenda ya kuonyesha michezo ya Ligi Kuu haikua na usawa, kampuni hiyo bado haijaanza hata matangazo, haijulikani ofisi zake zilipo, uwezo wa kurusha matangazo haujulikani kwa watanzania lakini bado wamepewa nafasi hyo.
Kikubwa tunamuomba rais wa TFF Leodgar Tenga kulitazama suala hili kwa umakini, kwani mtazamo wetu viongozi wa kamati ya Ligi wametazama maslahi yao binafsi bila kuzingatia uwezo wa timu na maliasili watu (wapenzi,washabiki).
Huwezi kuipa mgawo sawa timu ya Yanga na timu nyingine ambazo katika mechi zao binafsi wanatapata washabiki 50 kwenye mchezo, wakati Yanga imeongoza kwa mapato katika msimu mzima wa Ligi Kuu ya Vodacom na wastani wa washabiki 8,000 kwa kila mchezo.
Mwisho Makele amesema wanauamini uongozi uliopo na wapo nao bega kwa bega, tunaomba jamii nzima itambue kuwa Yanga inapigania haki zake na hao wote wanaobeza msimamo wetu basi wajibu hoja kwa hoja na sio kuongea tu pasipo kujibu hoja.

Monday, July 29, 2013

TAIFA STARS WAPIGWA 3-1 NA UGANDA THE CRANES



Tanzania (Taifa Stars) imeshindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa mara ya pili mfululizo baada ya leo (Julai 27 mwaka huu) kufungwa mabao 3-1 na Uganda Cranes, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1.
Stars ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009 ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao 1-1.
Wenyeji ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar. Frank Kalanda alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la Tanzania.
Bao hilo halikuonekana kuichangaza Taifa Stars, kwani ilitulia na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 mfungaji akiwa Amri Kiemba kutokana na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya eneo la mita 18.
Dakika ya 32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.
Mabao mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.
Kocha Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 43 kwa kumuingiza Simon Msuva badala ya Frank Domayo aliyeumia, na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo Haruni Chanongo na Vincent Barnabas badala ya David Luhende na John Bocco. Hata hivyo mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo.
Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani kesho (Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.

Wednesday, July 17, 2013

UKARABATI WA HOSTEL ZA COASTAL UNION



SHABIKI ALIKIMBIZA BASI LA ARSENAL




Shabiki mmoja raia wa Vetnam jana alifanya kitendo cha ajabu baada ya kukimbia sambamba na basi lilowabeba wachezaji wa Arsenal kwa takribani maili 3.


Katika kulikimbilia basi hilo alikutana na vigingi tofauti lakini kijana yule wa kivetnam hakukata tamaa ya kulifikia basi la Arsenal na kuwaona wachezaji wa timu aipendayo.

Baada ya kulikimbiza basi hilo kwa muda mrefu hatimaye kijana huyo alipata msaada kutoka kwa mwenye pikipiki na kuufikia mlango wa basi hilo na wachezaji wa Arsenal wakamfungulia mlango kisha kumpokea kwa furaha.

Kijana huyo alitimiza ndoto yake baada ya kupiga picha na wachezaji wote pamoja na kocha  Arsene Wenger.

ALCANTARA RASMI BAYERN MUNCHEN APEWA NAMBA 6



CAVANI RASMI MALI YA PSG




NAENDELEA KUBAKI NOU CAMP


Siku chache baada ya kumkosa Thiago Alcantara inaonekana sasa Manchester United ipo njiani kumkosa mchezaji mwingine kutoka FC Barcelona, Cesc Fabregas. Hii inakuja baada ya kocha wa klabu hiyo  Tito Vilanova kusema kwamba ameongea na kiungo huyo wa Spain na ameambia na mchezaji huyo kwamba anahitaji kuendelea kubaki Camp Nou.

Jana jumatatu iliripotiwa kwamba United walituma ofa ya kwanza ya kiasi cha £25.9 million  kwa ajili ya kumsajili Fabregas, ambaye amefeli kupata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu aliporudi akitokea Arsenal.

Lakini akiongea na waandishi wa habari leo mchana, Vilanova amesema wazi kwamba Fabregas bado anataka kubaki kwenye klabu yake hiyo ya utotoni, na hana mawazo ya kuondoka kwa sasa.
 "Ninafahamu kwamba tumepokea ofa kadhaa kutoka kwa vilabu tofauti. Niliongea na Cesc na ameniambia kwamba anataka kubaki.

"Cesc hana mawazo ya kuondoka kwenda klabu nyingine. Anajua ushindani ni mkubwa hapa na ana ndoto za kuendelea kuwa hapa na kufanikiwa.

Tuesday, July 16, 2013

OKWI ATOROKA TUNISIA



ETOILE du Sahel ya Tunisia inakusuduia kumshitaki mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa kuingia mitini katika klabu hiyo.
Okwi hajaonekana katika klabu hiyo kwa zaidi ya siku 30, na amekuwa akionekana akirandaranda katika mitaa ya jiji la Kampala, Uganda bila wasiwasi wowote.
Klabu hiyo ilimruhusu Okwi kujiunga na timu yake ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia, lakini tangu wacheze mechi dhidi ya Angola mjini Kampala Juni 15, mwaka huu, mshambuliaji huyo ameshindwa kurejea Tunisia na hajatoa taarifa yoyote.
Etoile du Sahel katika barua waliyomuandikia Okwi Julai 12 mwaka huu (Ijumaa iliyopita) na kusainiwa na Katibu Mkuu, Adel Ghith inasema kuwa iwapo straika huyo angekuwa hajarejea mpaka jana Jumatatu ingempeleka katika  vyombo husika vya sheria kwa hatua zaidi.
Katika barua hiyo, ambayo Mwanaspoti inayo, Katibu Mkuu wa Etoile du Sahel amemwambia Okwi kuwa licha ya kupigiwa simu mara kwa mara na makocha wa klabu hiyo tangu Juni 23, mchezaji huyo ameshindwa kuonyesha ushirikiano wowote.
“Ukiwa kama mchezaji profesheno, matendo yako yanachukuliwa kama kushindwa kuheshimu majukumu yako na ni kwenda kinyume na mkataba wako na klabu,” inasema sehemu ya barua hiyo.
Klabu hiyo imemkumbusha Okwi kuwa mkataba wake wa miaka mitatu utakwisha Julai 15, 2016 na kwamba kwa kutoripoti klabuni hapo ni kwenda kinyume na kifungu cha 2, 8 na 16 cha mkataba wake.
Katibu huyo katika barua hiyo amesema Okwi alikuwa amepewa mpaka jana Jumatatu awe ameripoti katika klabu hiyo vinginevyo atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufikishiwa katika vyombo husika vya kisheria.
Katibu huyo ameandika barua pepe nyingine mwishoni mwa wiki na kumkumbusha Okwi kuwa suala lake litafikishwa katika Shirikisho la Soka Tunisia (FTF) na Fifa.
Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) nalo limemuandika barua Okwi kumuonya kuhusu kitendo hicho.
“Jambo hili lipo ndani ya mamlaka yako na klabu. Fufa tulikuruhusu kuondoka ili urejee katika klabu yako, tunakusihi uheshimu kanuni za Fifa katika suala hili,” inasema barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Fufa, Edgar Waston Suubi.
Hata hivyo, habari ambazo Mwanaspoti inazo zinadai kuwa Okwi amegoma kujiunga na klabu yake kwa sababu haijamlipa baadhi ya fedha zake za kusaini pamoja na mshahara wa miezi mitatu.
Okwi aliuzwa na Simba kwa dola 300,000 (Sh 480 milioni), lakini klabu hiyo ya Msimbazi haijapata hata senti moja kwa madai kuwa Etoile du Sahel inapita katika kipindi kigumu na kwamba wanaweza kuwalipa Septemba.
Simu ya Okwi ilikuwa imezimwa jana Jumatatu, lakini watu wake wa karibu walisema alikuwa bado mjini Kampala.

YANGA YAMALIZA USAJILI NA OLOYA

 KOCHA wa Yanga, Ernie Brandts ametoa kauli ya mwisho kuwa anataka nafasi moja ya mwisho ya usajili wa wachezaji wa kigeni asajiliwe, Moses Oloya wa Uganda.
Ingawa amekiri kuwa amesikia mchezaji huyo anahitaji pesa nyingi lakini mambo yote amemwachia mkuu wake ambaye ni Mwenyekiti Kamati ya Usajili wa Yanga, Abdallah Bin Kleb.
Oloya ambaye anakipiga klabu ya Saigon Xuan Thanh, anatakiwa kwa udi na uvumba na Simba.
Na Oloya alipofanya mazungumzo na Mwanaspoti kutoka Vietnam alisema anamalizana na bosi wake wa Saigoni amkubalie aje Simba kabla ya mkataba wake kumalizika Oktoba wakati klabu hiyo ikiwa imebakiza mechi tano, lakini sasa Brandts kaagiza Yanga wafanye vurugu na kumleta kiungo huyo mshambuliaji Jangwani.
Akizungumza na Mwanaspoti jana Jumatatu, Brandts alisema: “Oloya ndiye mchezaji ninayemuhitaji kwa sasa, kawaida napenda mchezaji mzuri kama yeye ingawa nimesikia anahitaji pesa nyingi sana.
“Yanga hatuna tatizo sana kwa sababu kwa sasa, Kiiza (Hamis) amekuja na hawa wengine tulionao mambo yataenda vizuri,”
“Kama tutampata, Oloya tutamaliza kila kitu ingawa mambo hayo yote mkuu wangu, Bin Kleb ndiye anayeyafanyia kazi na anajua tutafanya nini,”alisisiza Brandts ambaye kwa sasa anao wachezaji Mrundi Didier Kavumbagu, Wanyarwanda Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite na Hamis Kiiza wa Uganda, ambaye alikuwa dakika za mwisho kumalizana na Yanga, hivyo kubakiwa na nafasi moja ya mchezaji wa kigeni.
Alipoulizwa kama atamkosa Oloya ni mchezaji wa aina gani anayemuhitaji, Brandts alisema kwa sababu hajajiunga na timu yoyote bado, hawezi kuzungumzia zaidi.
Kwa upande wa kambi ya Simba awali, Mwenyekiti Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe alisema wameshamalizana na Oloya na wamemwacha uhuru yeye mwenyewe amalizane na Saigoni ili atue Simba kabla ya msimu wa Ligi Kuu Bara kuanza.
Oloya mwenyewe alipozungumza na Mwanaspoti hivi karibuni alisema kuwa mipango yake ilikuwa ni kwenda Simba na akakiri kuwa amewahi kufanya mazungumzo na Yanga, lakini alikuwa amefika mbali zaidi na klabu ya Msimbazi kimazungumzo.
Hata hivyo, wachezaji hubadilika kama kinyonga, na ndio maana Mbuyu Twite alisaini mkataba wa Simba kabla ya kuruka kimanga na kutua Jangwani, hivyo suala la Oloya ni jambo la kusubiri mpaka dakika ya mwisho kujua atacheza Jangwani au Msimbazi.
Kocha wa Yanga ana historia katika ulimwengu wa soka akiwa anacheza beki ya kati ya taifa lake la Uholanzi alifunga mabao mawili kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1978 dhidi ya Italia, alifunga na kujifunga katika mechi hiyo hivyo matokeo kuwa 1-1.
Katika hatua nyingine, Brandts amezungumzia kambi ya kikosi chake na kusema anahitaji kambi nyingine ambayo atapata uwanja wenye sehemu nzuri ya kuchezea iwe ndani au nje ya nchi.
Alisema pia katika ziara ya Kanda ya Ziwa amepata mazoezi ya kutosha baada ya kucheza na Express wakatoa sare ya 1-1 kabla ya kufungwa 2-1 na baadaye wakatoka suluhu na Rhino ya Tabora.
“Hakuna tatizo kwenye kikosi changu ingawa kwa Tabora mazingira ya uwanja ndiyo hayakuwa mazuri,” alisema Brandts na kusisitiza washambuliaji wake ni wazuri ingawa wanakosa umakini kwenye kufunga.
Yanga haina mpango wa kuwachukua Kabange Twite na Yaw Berko katika usajili wa msimu huu, badala yake inataka straika

WAPINZANI WA USAIN BOLT WAKUTWA NA HATIA YA KUTUMIA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU



Wanariadha wawili kati ya wanariadha wenye kasi kubwa duniani Tyson Gay, kutoka Marekani na Asafa Powell wa Jamaica -- wamepatikana na kosa kutumia madawa ya kusisimua misuli.

Gay, ambaye ni mwanariadha wa pili kwa kuwa na kasi kubwa ya kukimbia katika mbio za mita mia moja, amesema anajiondoa kwenye mashindano ya dunia ya riadha yanayotarajiwa kufanyika mjini Moscow mwezi ujao.

Asafa Powell, ambaye alishikilia rekodi ya mbio za mita 100 hadi ilipovunjwa na Usain Bolt mwaka 2008, amekanusha kuwa alitumia dawa hizo makusudi.

Mwanariadha mwenzake wa Jamaica Sherone Simpson pia amepatikana na hatia ya kuzitumia dawa hizo za kusisimua misuli

EDINSON CAVANI ATUA PARIS KUFANYA VIPIMO VYA KUJIUNGA NA PSG


Cavani ametua rasmi jijini Paris Ufaransa tayari kufanyiwa vipimo vya afya baada ya Napoli kukubali ofa £55million kutoka kwa PSG. Endapo mchezaji huyo atafaulu vipimo basi atajiunga na PSG rasmi mapem kesho.