Pages

Saturday, August 31, 2013

ARSENAL HATA KAMA WANGEFUNGWA NA FENERBAHCE - BADO WANGEWEZA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA WA ULAYA

Klabu ya soka ya Uturuki, Fenerbahce, imepigwa marufuku ya kushiriki katika michuano ya bara Ulaya msimu huu, baada ya mahakama ya upatanishi ya michezo CAS, kuidhinisha uamuzi uliokuwa umetolewa na shirikisho la UEFA kuwa klabu hiyo ilihusika na sakata ya kupanga matokeo ya mechi.
Klabu hiyo ilikuwa, tayari kujiunga na ligi hiyo ya UEFA Cup, baada ya kuondolewa na Arsenal katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Shirikisho la UEFA, liliipiga marufuku Fenerbahce mwezi Juni mwaka huu, baada ya kuwapata maafisa wa klabu hiyo na hatia ya kupanga matokeo ya mechi ili kushinda ligi kuu ya soka nchini Uturuki.

Kwa maana hiyo hata kama wangefanikiwa kuitoa Arsenal katika mechi ya kufuzu champions league isingekuwa na maana kwao kutokana kufungiwa huko.

MAN UNITED YATUMA OFA YA £25M KWA ANDER HERRERA YAPIGWA CHINI - AS ROMA YAGOMA KUFUNGUA NAO MAZUNGUMZO JUU YA USAJILI WA DE ROSSI

Inaonekana klabu ya Manchester United ina bahati mbaya katika soko la usajili la wakati huu baada ya leo hii ofa ya £25million kwenda Atheltic Bilbao kwa ajili ya kumsajili Ander Herrera kupigwa chini - huku Roma wakigoma hata kuanzisha mazungumzo juu ya usajili wa Daniele De Rossi.

Kiungo mwenye miaka 24 wa kihispania, Herrera, aliwavutia United kwa muda mrefu sasa tangu Bilabo ilipowachakaza United katika Europa League misimu iliyopita.

Na De Rossi, 30, mshindi wa kombe la dunia ambaye ameshaichezea mechi 91 Italy na mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa na wanaolipwa fedha nyingi katika Serie A.

Raisi wa Bilbao Jose Urrutia alikaririwa akisema kwenye mtandao wa Twitter: 'Kuna ofa imetumwa kwa ajili ya Ander Herrera. Tumeipokea jana na tumejibu kwamba hatuna mpango wa kuuza wachezaji wetu.
'Klabu yetu ni tofauti. Tunajenga mahusiano ya kihisia na wachezaji wetu. Kwetu fedha sio jambo muhimu sana, ikitokea mchezaji anataka kuondoka basi inabidi aseme na klabu inayomtaka ilipe kiasi ambacho kimepangwa kwenye mkataba.'

Wakati huo huo Moyes ameshindwa kukanusha kwamba walituma kwa Herrera lakini akasema kamba ana matumaini ya kuongeza wachezaji kwenye kikos chake.
'Ninatumaini tutafanya baishara ya ununuzi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.'

SAMUEL ETO'O RASMI CHELSEA



YANGA ILIVYOVUTWA SHATI NA WAGOSI WA KAYA COASTAL UNION UWANJA WA TAIFA


Waamuzi wa leo wakiwa na manahodha wa timu zote mbili Jerry Santo wa Coastal Union na Nadir Haroub wa Yanga.
 Uhuru Suleiman akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Yanga kwenye mechi ya leo iliyoisha kwa suluhu ya 1-1.
Haruna Moshi 'Boban akipambana na Cannavaro
 Kimenukaaaaaaaa mashabiki wa Wagosi wa kaya kutoka Tanga moja kwa moja mpaka uwanjani, na kutoka uwanjani moja kwa moja mpaka Tanga. Ama kweli waja leo waondoka leo.(PICHA KWA HISANI YA COASTAL UNION BLOG)
                         Kikosi cha leo hiki kilichoanza dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
  
Hamad Juma akitafuta mbinui za kumtoka mchezaji wa Ynga, Mbuyu Twite huku Crispin Odula akiwa tayari kumsaidia.
                   Hapa Nadir Haroub akijaribu kumdhibiti 'toto tundu' Yayo Kato lakini alishindwa.
Abdi Banda kati kati ya wachezaji wa Yanga.
                             'Selembe' Suleiman Kassim akizongwa na Juma Abdul (12) wa Yanga.
Kulitokea tafrani kidogo wachezaji wa Yanga na Coastal Union, hatimaye mwamuzi akatoa kadi nyekundu kwa wachezaji wawili Odula (Coastal Union) na Simon Msuva (Yanga).
 Hii ndiyo penalt aliyofunga Jerry Santo dakika ya 90 baada ya David Luhende wa Yanga kuunawa mpira eneo la hatari.
                                                            

 

ARSENE WENGER AMRUDISHA RASMI FLAMINI KWA MKATABA WA MIAKA 3

 

Arsene Wenger amefanya usajili wa pili katika dirisha hili la usajili linaloelekea mwishoni kwa kumsajili kiungo wa zamani wa timu Mathieu Flamini kwa uhamisho wa bure kutoka AC Milan.

Kiungo huyo ambaye aliondoka Gunners mwaka 2008 kujiunga na  AC Milan, amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya  £40,000 kwa wiki.
Flamini, 29, ni mchezaji wa pili kusajiliwa baada ya mshambuliaji kinda wa kifaransa Yaya Sanogo, ambaye amejiunga na Arenal akitokea Auxerre bure. 

Flamini amekuwa akifanya mazoezi na Arsenal wakati wote wa pre season baada ya kuachwa na AC Milan mwishoni mwa msimu uliopita. 

Sunday, August 25, 2013

MATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM: SIMBA YAVUTWA SHARUBU - YANGA YAUA.

Matokeo kamili ya Ligi Kuu Tanzania

Mtibwa Sugar 1 - 1 Azam FC
Rhino Rangers 2 - 2 Simba SC
Coastal Union 2 - 0 JKT Oljoro
Mbeya City 0 - 0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 3 - 0 Tanzania Prisons
Young Africans 5 - 1 Ashanti United.

CHELSEA YATHIBITISHA RASMI KUMSAJILI WILLIAN.

Chelsea imethibitisha kwamba imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo Willian kutoka Anzhi Makhachkala.

The Blues wameshindwa kutoa taarifa rasmi ya ada ya uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri miaka 25, lakini ripoti zinasema watailipa klabu ya Russia kiasi cha £32million.

Tottenham walikuwa wanakaribia kumsajili mbrazil huyo, wakiwa tayari wameshakubaliana bei na Anzhi na hata vipimo vya afya vilishafanyika. 

Lakini wakati wakiwa bado wanabishana kuhusu maslahi binafsi ya mchezaji, wawakilishi wa kiungo huyo wa kibrazil wakatoa ofa kwa Chelsea kumsajili kiungo huyo ambaye klabu hiyo ya London imekuwa ikimuwinda kwa muda mrefu.

Taarifa kutoka kwenye mtandao rasmi wa Chelsea inasomeka:  "Chelsea Football Club inaweza kuthibitisha kwamba imefikia makubaliano na Willian pamoja na klabu ya Anzhi Makhachkala kwa uhamisho wa mchezaji huyo wa kibrazil

Kilichobakia sasa ni kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza ambacho kinategemewa kutoka jumatano ijayo."
 
Willian anakuwa mchezaji tatu kusajiliwa na Chelsea kwenye dirisha hili la usajili, kufuatia kuwasili kwa  Andre Schurrle kutoka Bayer Leverkusen na Marco van Ginkel kutoka Vitesse Arnhem, wakati huo Wayne Rooney akiwa bado ni kipaumbele kikuu katika usajili wa upande wa mshambuliaji.

HARUNA MOSHI BOBAN - KADO WANG'ARA COASTAL UNION IKIWAUA OLJORO 2-0 ARUSHA

 Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Hilal 'Aurora' akisalimiana na Yayo Kato, kabla ya mpira kuanza.

                                         Kikosi cha leo hiki kilichoanza dhidi ya Oljoro JKT.




                         Yayo Kato akituliza mpira mbele ya Majaliwa Mbaga wa JKT Oljoro.

 Mashabiki wa Coastal Union waliuteka uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo. Watu wote mazungumzo ni kigoma hiki.

 Yusuf Machogote wa JKT Oljoro akijaribu kukimbilia mpira na Suleiman Selembe leo.

 Hiki ni kipindi cha pili Selembe alikosa bao la wazi yeye na golikipa. Na hili lilikuwa bao la pili kukosa baada ya kipindi cha kwanza kupewa pasi murua na Yayo akabaki na golikipa akapiga kichwa mpira ukatoka nje.

 Uhuru Suleiman akijaribu kutafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Oljoro leo.

 Selembe akimpongeza Abdi Banda baada ya kufunga bao la kwanza ndani ya dakika 16 ya mchezo.

 Hapa Banda akiwa anarudi kutoka kufurahia na mashabiki wa Coastal Union waliofurika uwanjani leo.

 Mwamuzi wa leo kutoka Mwanza Jacob Adengo akimwonyesha kadi ya Njano Banda kwa kutoka nje ya uwanja wakati mpira ukiendelea.

 Shaaban Kado leo alikuwa nyota ya mchezo baada ya kuopoa michomo mingi ambayo iliyawacha watu mdomo wazi.

 Hapa mashabiki wa Oljoro wakiingia uwanjani kipindi cha pili baada ya kupigiwa simu waje kuongeza nguvu maana kigoma cha Wagosi kiliwazidi nguvu.

                                                 Morocco akisisitiza jambo uwanjani.



               Haruna Moshi Boban leo alivutia watu wengi kutokana na style yake ya kucheza.

 Hamad 'Basmat' akikokota mpira bila wasiwasi wowote, leo alipiga beki nzuri hakuna mchezji aliyethubutu kumsogelea.

                                                Selembe akituliza mpira kwa ufundi mkubwa.

                         Haruna Moshi 'Boban' akituliza mpira mbele ya wachezaji wawili wa Oljoro.


              Mashabiki wa Coastal Union baada ya mpira kuisha ilikuwa raha tu mwanzo mwisho.

Nassor Binslum, Akida Machai na Heme Hilal wakiwa katika viunga vya jiji la Arusha baada ya mechi kuisha kwa ushindi 2-0.

PICHA ZIKIONESHA YANGA ILIPOIBANDIKA ASHANTI GOLI 5-1.

 Wachezaji wa Ashanti United wakisalimiana na wachezaji wa Yamnga kabla ya mchezo. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Beki wa Ashanti United, Ramadhani Malima akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Hussein Javu, katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda 5-1. 
Wachezaji wa Yanga wakiwa katika ya pamoja.
 Beki wa Ashanti United, Emanuel Kichiba (kushoto), akichuana na kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 5-1.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi wa bao 5-1.

BAADA YA JANA KUANZA KUUZA JEZI ZAKE - LEO HII REAL MADRID WAANZA KUTENGENEZA JUKWAA

Gareth Bale anakaribia kutua Real Madrid

BSW25jqIgAAKTWM {Pictures} Real Madrid preparing stage for tomorrows presentation of Gareth Bale [AS]
Ujeniz wa jukwaa kubwa la kutambulishia wachezaji wakubwa wanaosajiliwa na Real Madrid ukiendelea mapema jana mchana. Inaaminika Real Madrid wapo katika hatua za mwisho za kumsajili Gareth Bale kwa ada ya uhamisho wa £94m ambayo itakuwa rekodi mpya ya dunia baada ya ile £80m waliyolipa Madrid kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United miaka minne iliyopita.
Miaka minne iliyopita Cristiano Ronaldo alikuwa mtu wa mwisho kupita juu ya jukwaa hili - na kama habari zilizopo ni za kuaminika basi Gareth Bale akiwa na jezi yake namba 11 atakuwa mchezaji mwingine kutoka ligi kuu ya Uingereza kupanda kwenye jukwaa ndani ya uwanja wa Santiago Bernabeu ndani ya siku chache zijazo

BSW3fY9CcAE8LT0 {Pictures} Real Madrid preparing stage for tomorrows presentation of Gareth Bale [AS]