Pages

Wednesday, November 27, 2013

USAJILI DIRISHA DOGO KUFUNGWA DESEMBA 15 - KUANZIA MSIMU UJAO WACHEZAJI WA KIGENI MWISHO WA 3 KWA KILA TIMU

Wakati dirisha dogo la usajili linafungwa Desemba 15 mwaka huu, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunazikumbusha klabu zote kuheshimu kanuni na kuzingatia muda uliowekwa.
Pia tunakumbusha kuwa kupeleka mchezaji kwa mkopo katika klabu nyingine hakutoi nafasi ya kusajili mchezaji mpya. Kama klabu ilisaji wachezaji 30 maana yake ni kuwa haina nafasi ya kuongeza wachezaji.
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni (foreign players), tunakumbusha kuwa kuanzia msimu ujao 2014/2015 watakuwa watatu tu badala ya watano wa sasa.
Kuhusu usajili wa wachezaji kutoka nje mpaka sasa hakuna hata klabu moja imeshaingia kwenye TMS kuomba uhamisho. Itakapofika Desemba 15, system ya TMS itafunga.

KOMBE LA CHALLENJI: ZANZIBAR HEROES KUFUNGUA MICHUANO NA SUDAN YA KUSINI KESHO



Michuano mikongwe barani Afrika ya kombe la Challenge kwa nchi za ukanda wa Afrika ya mashariki na kati Cecafa inatarajiwa kuanza hapo kesho kwenye viwanja vya Nyayo jijini Nairobi na Machakos nchini Kenya, kwa jumla ya nchi kumi na mbili kuwania taji hilo.
Wenyeji Harambee starz ya Kenya, machampioni watetezi wa taji Uganda The Creans, Walya Antelope ya Ethiopia, Ocean boyz wa Somalia, Zanzibar Heroes ya Tanzania visiwani, Kilimanjaro starz ya Tanzania bara, Sudani ya kusini na ile ya Kaskazini, zinamenyanya.
Nyingine ni pamoja na Eritrea, Intamba Murugamba ya Burundi, Amavubi ya Rwanda, na waalikwa kwenye michuano hiyo Askari wa Chipolopolo toka nchini Zambia, zinawania taji hilo.
Timu zimegawanywa kwenye makundi ya A,B na C, ambapo kundi la A wapo Zanzibar Heroes ya Zanzibar, Walya Antelope ya Ethiopia, Sudan ya Kusini, na wenyeji Harambee starz ya Kenya, watasaka nafasi mbili za juu kucheza robo fainali.
Kundi la pili, lina timu za Kilimanjaro starz ya Tanzania bara, Chipolopolo ya Zambia, Intamba Murugamba ya Burundi, na mabaharia wa Somalia.
Kundi la tatu ambalo ni la C, lina timu za Amavubi ya Rwanda, machampioni watetezi wa taji Uganda the Creans, Sudan ya Kaskazini na mabaharia a Somalia.
Mechi za ufunguzi za michuano hiyo zinatarajiwa kuanza kesho kwa michezo baina ya wenyeji Harambee starz ya Kenya dhidi ya Walya Antelope ya Ethiopia kwenye uwanja wa Nyayo, lakini kabla utapigwa mchezo baina ya Zanzibar Heroes dhidi ya Sudani ya kusini.

Tuesday, November 26, 2013

JEZI MPYA ZA BRAZILI ZA KUCHEZEA KOMBE LA DUNIA 2014.





CHUJI, CANNAVARO, MSUVA NA JERRY TEGETE WAONGEZA MIKATABA YANGA - KUBAKI JANGWANI MPAKA 2016

Wachezaji watano wa timu ya Young Africans wameongeza mikataba ya muda mrefu ambapo sasa wataendelea kuitumikia klabu yenye maskani yake mitaa ya Twiga/Jangwani mpaka mwaka 2016, hili limefanywa na uongozi kwa mapendekezo ya benchi la ufundi.

Wachezaji ambao mpaka sasa wameshaongeza mikataba ya kuitumikia klabu ya Young Africans ni walinzi Kelvin Yondani (2014-2016), Nadir Haroub "Cannavaro" (2014-2016), kiungo Athuman Idd (2014-2016), mshambuliaji Saimon Msuva (2014-2016) na Jerson Tegete (2014-2016).

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb amesema hao ni baadhi tu ya wachezaji ambao wameshamaliza taratibu zote na kusaini mikataba mipya itakayowafanya waitumikie Yanga mpaka mwaka 2016.

"Tupo katika mazungumzo ya mwisho na wachezaji wetu wengine, mazungumzo yanaendelea vizuri na tunaamini muda si mrefu nao tutakua tumeshamalizana nao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga tena kwa muda mrefu "alisema Bin Kleb.

Wakati huo huo kikosi cha Young Africans leo kimeanza mazoezi asubuhi katika uwanja wa Bora - Mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo wa hisani dhidi ya Simba SC Disemba 14, 2013, mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.

SOURCE: YANGA WEBSITE

RONALDO AONGOZA KWENYE KUWANIA UCHEZAJI BORA WA DUNIA.

Thursday, November 14, 2013

FUTURE YOUNG TAIFA STARS YAICHAPA TAIFA STARS 1-0.

Mshambulia wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa (kulia) akichuana na mchezaji wa Future Young Taifa Stars, Kabanda katika mchezo kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Kiungo wa Taifa Stars, Athuma Idd "Chuji" akichuana na mchezaji wa Future Young Taifa Stars,Paul Nonga.
Beki wa Stars Erasto Nyoni (kushoto), akichuana na mshambuliaji wa Future Young Taifa Stars, Simon Msuva.
Erasto Nyoni akipimana ubavu na Simon Msuva.
Chuji akimtoka Paul Nonga.
Uniwezi bwana mdogo......Chuji akichuana na Paul Nonga wa Future Young Taifa Stars.
Makocha wakijadiliana jambo wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wakishuhudia mechi hiyo kupitia katika jengo la Machinga Complex.
Msuva akitoka baada ya kuumia.
Moja ya hekaheka.

KIM ATEUA 32 KUIKABILI KENYA.



Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
Wachezaji walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

RAISI WA BAYERN MUNICH AMWAGA CHOZI AKITANGAZA KUTENGENEZA FAIDA KUBWA ZAIDI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 113


Raisi wa Bayern Munich Uli Hoeness, anakabiriwa na kesi ya kukwepa kodi itakasomwa mwakani, jana alitokwa na machozi wakati akitangaza klabu yake kuvunja rekodi ya kuingiza mapato makubwa katika cha 113 years.
Katika mkutano wa mkuu wa klabu, Hoeness, ambaye alipokewa kwa shangwe, alishindwa kujizuia na kuanza kulia baada ya mabosi wenzie kumsifia kuiongoza vizuri timu hiyo na kupata mafanikio ya kushinda makombe matatu msimu uliopita. 
Hoeness, ambaye anashtakiwa kwa kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye fedha zake zilizopo katika moja ya benki huko Uswis.
 
Hoeness, amekuwa katika klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 40 kama mchezaji, kocha na saa raisi, alizungumzia matatizo yake ya kisheria, akisema kwamba alifanya makosa na kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye akaunti yake ya nje.
'Nilifanya makosa kutokulipa kodi katika uwekezaji kutoka nje. Sikuchukua mamilioni ya fedha na kuyatoa nje ya nchi," alisema Hoeness, baada ya kujifuta machozi.  'Nitapambana na matatizo.'
'Nina imani kubwa na utawala wa kisheria wa Bavarian.
'Ninatumaini kwamba story hii itakuwa na mwisho mzuri mpaka kufikia mwezi  March. Na kama mpaka wakati huo nitaruhusiwa kuendelea kuwa hapa naahidi kuitumikia klabu hii mpaka pumzi yangu ya mwisho.'

HUYU NDIO MCHEZAJI MWINGINE ALIYESAJILIWA NA YANGA BAADA YA KASEJA.


Monday, November 11, 2013

TUZO ZA MWANASOKA BORA WA TANZANIA: HARUNA NIYONZIMA AIBUKA KIDEDEA, AWABWAGA KIEMBA NA YONDANI.

Hii ndio ilikuwa kamati iliyoratibu tuzo hizo :Zamoyoni Mogella ( Mwenyekiti ), Kenny Mwaisabula ( Kaimu katibu ), na wajumbe Shaffih Dauda, Boniface Wambura,Edo Kumwembe na Doris Malyaga.

  Godfrey Nyange akimkabidhi tuzo mwaamuzi bora Oden Mbaga.
Ezekiel Kamwaga akipokea  tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa niaba ya Abdallah Kibadeni.
Zamoyoni Mogella akitoa tuzo ya bao la mwaka kwa mwakilishi wa Thomas Ulimwengu.

Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga kushoto akimkabidhi tuzo ya Ufungaji Bora mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast katika tuzo za gazeti la Mwanaspoti usiku wa jana ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.




Kiungo wa Simba Amri Kiemba akipokea tuzo ya 11 Bora





Niyonzima akikabidhiwa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka.
Haruna Niyonzima akikabidhiwa zawadi yake ya kuwa mwanasoka bora wa Tanzania




  Haruna Shamte ( kushoto ),Ramadhani Singano pamoja na mdau.


 
Joseph Kimwaga wa Azam Fc ndiye alichukua tuzo ya mwanasoka chipukizi.


Rais wa zamani wa SAFA,Kirsten Nematandani akimpatia tuzo Haruna Niyonzima ya mwanaoka bora wa kigeni wa mwaka.
Juma Nature Kibla akitumbuiza kwenye tuzo hizo


Rais wa heshima wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Said El Maamry akimkabidhi tuzo ya Mchezaji bora wa Tanzania anayecheza nje, mwakilishi wa mshindi wa tuzo hiyo, Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya DRC