Pata habari za michezo katika blog hii na kujua maisha ya wachezaji wa ndani na nje.
Thursday, August 01, 2013
XAVI: "BALE SIO WA THAMANI YA MILLIONI 90 - CESC FABREGAS BADO ANA FURAHA CAMP NOU"
Kiungo huyo wa Hispania amenukuliwa
akisema kwamba bado hajamuangalia vizuri nyota huyo wa Spurs kiasi cha
kumfanya kutoa maoni yake kuhusu kutakiwa kwake na Real Madrid.
Alisema: “Sidhani kama Bale ana thamani ya fedha hizo zinazotajwa.
“Kiukweli kabisa sijawahi kumuona akicheza dakika 90 zote.”
Xavi pia alisisitiza Cesc Fabregas ana furaha kuwepo ndani ya Barcelona, pamoja na kutakiwa na Manchester United.
Kiungo huyo alisema: “Anaonekana kutulia, ana mkataba hapa. Anajituma mazoezini na anacheza vizuri.
"Kuhusu kuondoka, nadhani ni tetesi tu. Tutaona kitakachotokea lakini kwa sasa anaonekana kutulia na tayari kwa msimu mpya na Barcelona.”
Alisema: “Sidhani kama Bale ana thamani ya fedha hizo zinazotajwa.
“Kiukweli kabisa sijawahi kumuona akicheza dakika 90 zote.”
Xavi pia alisisitiza Cesc Fabregas ana furaha kuwepo ndani ya Barcelona, pamoja na kutakiwa na Manchester United.
Kiungo huyo alisema: “Anaonekana kutulia, ana mkataba hapa. Anajituma mazoezini na anacheza vizuri.
"Kuhusu kuondoka, nadhani ni tetesi tu. Tutaona kitakachotokea lakini kwa sasa anaonekana kutulia na tayari kwa msimu mpya na Barcelona.”
SAKATA LA YANGA KUPINGA MECHI ZAO KUONYESHWA AZAM TV WANACHAMA WA KLABU WAUNGA MKONO
Uongozi wa matawi wa klabu ya Yanga (wenyeviti na makatibu) leo
umefanya kikao katika makao makuu ya klabu mtaa wa twiga/jangwani kisha
kutoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuhusiana na tamko la uongozi
(kamati ya utendaji) kutokubali kuonyeshwa kwa michezo yake kwenye
luninga.
Awali klabu ya Yanga juzi kupitia kamati ya utendaji ilifanya mkutano na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa klabu kuhusiana na kutoridhishwa na kamati ya muda ya Ligi (TPL) kuingia makubaliano ya kurushwa matangazo ya televsheni kwenye michezo yake.
Akiongea na waandishi wa habari leo katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako alisema baada ya kukaa na viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga jijni Dar es salaam kwa pamoja wamekubali na kuunga mkono hoja zilizowasilisha na viongozi juu ya haki ya matangazo.
Mmoja wa viongozi wa matawi Bakili Makele akiongea kwa niaba ya viongozi wa matawi, alisema TFF inaamua kukandamiza soka la Tanzania kwa kuviamulia maamuzi yake juu ya kuonyeshwa kwa michezo ya timu kwenye luninga.
Makele amesema taratibu za kuipa kampuni ya Azam TV tenda ya kuonyesha michezo ya Ligi Kuu haikua na usawa, kampuni hiyo bado haijaanza hata matangazo, haijulikani ofisi zake zilipo, uwezo wa kurusha matangazo haujulikani kwa watanzania lakini bado wamepewa nafasi hyo.
Kikubwa tunamuomba rais wa TFF Leodgar Tenga kulitazama suala hili kwa umakini, kwani mtazamo wetu viongozi wa kamati ya Ligi wametazama maslahi yao binafsi bila kuzingatia uwezo wa timu na maliasili watu (wapenzi,washabiki).
Huwezi kuipa mgawo sawa timu ya Yanga na timu nyingine ambazo katika mechi zao binafsi wanatapata washabiki 50 kwenye mchezo, wakati Yanga imeongoza kwa mapato katika msimu mzima wa Ligi Kuu ya Vodacom na wastani wa washabiki 8,000 kwa kila mchezo.
Mwisho Makele amesema wanauamini uongozi uliopo na wapo nao bega kwa bega, tunaomba jamii nzima itambue kuwa Yanga inapigania haki zake na hao wote wanaobeza msimamo wetu basi wajibu hoja kwa hoja na sio kuongea tu pasipo kujibu hoja.
Awali klabu ya Yanga juzi kupitia kamati ya utendaji ilifanya mkutano na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa klabu kuhusiana na kutoridhishwa na kamati ya muda ya Ligi (TPL) kuingia makubaliano ya kurushwa matangazo ya televsheni kwenye michezo yake.
Akiongea na waandishi wa habari leo katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako alisema baada ya kukaa na viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga jijni Dar es salaam kwa pamoja wamekubali na kuunga mkono hoja zilizowasilisha na viongozi juu ya haki ya matangazo.
Mmoja wa viongozi wa matawi Bakili Makele akiongea kwa niaba ya viongozi wa matawi, alisema TFF inaamua kukandamiza soka la Tanzania kwa kuviamulia maamuzi yake juu ya kuonyeshwa kwa michezo ya timu kwenye luninga.
Makele amesema taratibu za kuipa kampuni ya Azam TV tenda ya kuonyesha michezo ya Ligi Kuu haikua na usawa, kampuni hiyo bado haijaanza hata matangazo, haijulikani ofisi zake zilipo, uwezo wa kurusha matangazo haujulikani kwa watanzania lakini bado wamepewa nafasi hyo.
Kikubwa tunamuomba rais wa TFF Leodgar Tenga kulitazama suala hili kwa umakini, kwani mtazamo wetu viongozi wa kamati ya Ligi wametazama maslahi yao binafsi bila kuzingatia uwezo wa timu na maliasili watu (wapenzi,washabiki).
Huwezi kuipa mgawo sawa timu ya Yanga na timu nyingine ambazo katika mechi zao binafsi wanatapata washabiki 50 kwenye mchezo, wakati Yanga imeongoza kwa mapato katika msimu mzima wa Ligi Kuu ya Vodacom na wastani wa washabiki 8,000 kwa kila mchezo.
Mwisho Makele amesema wanauamini uongozi uliopo na wapo nao bega kwa bega, tunaomba jamii nzima itambue kuwa Yanga inapigania haki zake na hao wote wanaobeza msimamo wetu basi wajibu hoja kwa hoja na sio kuongea tu pasipo kujibu hoja.
Monday, July 29, 2013
TAIFA STARS WAPIGWA 3-1 NA UGANDA THE CRANES
Tanzania
(Taifa Stars) imeshindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa
Ndani (CHAN) kwa mara ya pili mfululizo baada ya leo (Julai 27 mwaka
huu) kufungwa mabao 3-1 na Uganda Cranes, hivyo kutolewa kwa jumla ya
mabao 4-1.
Stars
ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009
ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa
Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao
1-1.
Wenyeji
ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo
iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar. Frank Kalanda
alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la
Tanzania.
Bao
hilo halikuonekana kuichangaza Taifa Stars, kwani ilitulia na
kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 mfungaji akiwa Amri Kiemba kutokana
na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya eneo la mita 18.
Dakika
ya 32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho
Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba
kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.
Mabao
mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian
Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na
makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi
nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.
Kocha
Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 43 kwa kumuingiza Simon Msuva
badala ya Frank Domayo aliyeumia, na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo
Haruni Chanongo na Vincent Barnabas badala ya David Luhende na John
Bocco. Hata hivyo mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo.
Kikosi
cha Stars kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David
Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd,
Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo,
Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani kesho
(Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.
Wednesday, July 17, 2013
SHABIKI ALIKIMBIZA BASI LA ARSENAL
Shabiki mmoja raia wa Vetnam jana alifanya kitendo cha ajabu baada ya kukimbia sambamba na basi lilowabeba wachezaji wa Arsenal kwa takribani maili 3.
Katika
kulikimbilia basi hilo alikutana na vigingi tofauti lakini kijana yule
wa kivetnam hakukata tamaa ya kulifikia basi la Arsenal na kuwaona
wachezaji wa timu aipendayo.
Baada
ya kulikimbiza basi hilo kwa muda mrefu hatimaye kijana huyo alipata
msaada kutoka kwa mwenye pikipiki na kuufikia mlango wa basi hilo na
wachezaji wa Arsenal wakamfungulia mlango kisha kumpokea kwa furaha.
Kijana huyo alitimiza ndoto yake baada ya kupiga picha na wachezaji wote pamoja na kocha Arsene Wenger.
NAENDELEA KUBAKI NOU CAMP
Siku
chache baada ya kumkosa Thiago Alcantara inaonekana sasa Manchester
United ipo njiani kumkosa mchezaji mwingine kutoka FC Barcelona, Cesc Fabregas. Hii inakuja baada ya kocha wa klabu hiyo Tito Vilanova kusema kwamba ameongea na kiungo huyo wa Spain na ameambia na mchezaji huyo kwamba anahitaji kuendelea kubaki Camp Nou.
Jana jumatatu iliripotiwa kwamba United walituma ofa ya kwanza ya kiasi cha £25.9 million kwa ajili ya kumsajili Fabregas, ambaye amefeli kupata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu aliporudi akitokea Arsenal.
Lakini akiongea na waandishi wa habari leo mchana, Vilanova amesema wazi kwamba Fabregas bado anataka kubaki kwenye klabu yake hiyo ya utotoni, na hana mawazo ya kuondoka kwa sasa.
"Ninafahamu kwamba tumepokea ofa kadhaa kutoka kwa vilabu tofauti. Niliongea na Cesc na ameniambia kwamba anataka kubaki.
"Cesc hana mawazo ya kuondoka kwenda klabu nyingine. Anajua ushindani ni mkubwa hapa na ana ndoto za kuendelea kuwa hapa na kufanikiwa.
Jana jumatatu iliripotiwa kwamba United walituma ofa ya kwanza ya kiasi cha £25.9 million kwa ajili ya kumsajili Fabregas, ambaye amefeli kupata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu aliporudi akitokea Arsenal.
Lakini akiongea na waandishi wa habari leo mchana, Vilanova amesema wazi kwamba Fabregas bado anataka kubaki kwenye klabu yake hiyo ya utotoni, na hana mawazo ya kuondoka kwa sasa.
"Ninafahamu kwamba tumepokea ofa kadhaa kutoka kwa vilabu tofauti. Niliongea na Cesc na ameniambia kwamba anataka kubaki.
"Cesc hana mawazo ya kuondoka kwenda klabu nyingine. Anajua ushindani ni mkubwa hapa na ana ndoto za kuendelea kuwa hapa na kufanikiwa.
Tuesday, July 16, 2013
OKWI ATOROKA TUNISIA

Okwi hajaonekana katika klabu hiyo kwa zaidi ya
siku 30, na amekuwa akionekana akirandaranda katika mitaa ya jiji la
Kampala, Uganda bila wasiwasi wowote.
Klabu hiyo ilimruhusu Okwi kujiunga na timu yake
ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia,
lakini tangu wacheze mechi dhidi ya Angola mjini Kampala Juni 15, mwaka
huu, mshambuliaji huyo ameshindwa kurejea Tunisia na hajatoa taarifa
yoyote.
Etoile du Sahel katika barua waliyomuandikia Okwi
Julai 12 mwaka huu (Ijumaa iliyopita) na kusainiwa na Katibu Mkuu, Adel
Ghith inasema kuwa iwapo straika huyo angekuwa hajarejea mpaka jana
Jumatatu ingempeleka katika vyombo husika vya sheria kwa hatua zaidi.
Katika barua hiyo, ambayo Mwanaspoti inayo, Katibu
Mkuu wa Etoile du Sahel amemwambia Okwi kuwa licha ya kupigiwa simu
mara kwa mara na makocha wa klabu hiyo tangu Juni 23, mchezaji huyo
ameshindwa kuonyesha ushirikiano wowote.
“Ukiwa kama mchezaji profesheno, matendo yako
yanachukuliwa kama kushindwa kuheshimu majukumu yako na ni kwenda
kinyume na mkataba wako na klabu,” inasema sehemu ya barua hiyo.
Klabu hiyo imemkumbusha Okwi kuwa mkataba wake wa
miaka mitatu utakwisha Julai 15, 2016 na kwamba kwa kutoripoti klabuni
hapo ni kwenda kinyume na kifungu cha 2, 8 na 16 cha mkataba wake.
Katibu huyo katika barua hiyo amesema Okwi alikuwa
amepewa mpaka jana Jumatatu awe ameripoti katika klabu hiyo vinginevyo
atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufikishiwa katika vyombo
husika vya kisheria.
Katibu huyo ameandika barua pepe nyingine mwishoni
mwa wiki na kumkumbusha Okwi kuwa suala lake litafikishwa katika
Shirikisho la Soka Tunisia (FTF) na Fifa.
Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) nalo limemuandika barua Okwi kumuonya kuhusu kitendo hicho.
“Jambo hili lipo ndani ya mamlaka yako na klabu.
Fufa tulikuruhusu kuondoka ili urejee katika klabu yako, tunakusihi
uheshimu kanuni za Fifa katika suala hili,” inasema barua iliyoandikwa
na Katibu Mkuu wa Fufa, Edgar Waston Suubi.
Hata hivyo, habari ambazo Mwanaspoti inazo zinadai
kuwa Okwi amegoma kujiunga na klabu yake kwa sababu haijamlipa baadhi
ya fedha zake za kusaini pamoja na mshahara wa miezi mitatu.
Okwi aliuzwa na Simba kwa dola 300,000 (Sh 480 milioni), lakini
klabu hiyo ya Msimbazi haijapata hata senti moja kwa madai kuwa Etoile
du Sahel inapita katika kipindi kigumu na kwamba wanaweza kuwalipa
Septemba.
Simu ya Okwi ilikuwa imezimwa jana Jumatatu, lakini watu wake wa karibu walisema alikuwa bado mjini Kampala.
YANGA YAMALIZA USAJILI NA OLOYA
KOCHA wa Yanga, Ernie Brandts ametoa kauli ya mwisho kuwa
anataka nafasi moja ya mwisho ya usajili wa wachezaji wa kigeni
asajiliwe, Moses Oloya wa Uganda.
Ingawa amekiri kuwa amesikia mchezaji huyo
anahitaji pesa nyingi lakini mambo yote amemwachia mkuu wake ambaye ni
Mwenyekiti Kamati ya Usajili wa Yanga, Abdallah Bin Kleb.
Oloya ambaye anakipiga klabu ya Saigon Xuan Thanh, anatakiwa kwa udi na uvumba na Simba.
Na Oloya alipofanya mazungumzo na Mwanaspoti
kutoka Vietnam alisema anamalizana na bosi wake wa Saigoni amkubalie aje
Simba kabla ya mkataba wake kumalizika Oktoba wakati klabu hiyo ikiwa
imebakiza mechi tano, lakini sasa Brandts kaagiza Yanga wafanye vurugu
na kumleta kiungo huyo mshambuliaji Jangwani.
Akizungumza na Mwanaspoti jana Jumatatu, Brandts
alisema: “Oloya ndiye mchezaji ninayemuhitaji kwa sasa, kawaida napenda
mchezaji mzuri kama yeye ingawa nimesikia anahitaji pesa nyingi sana.
“Yanga hatuna tatizo sana kwa sababu kwa sasa, Kiiza (Hamis) amekuja na hawa wengine tulionao mambo yataenda vizuri,”
“Kama tutampata, Oloya tutamaliza kila kitu ingawa
mambo hayo yote mkuu wangu, Bin Kleb ndiye anayeyafanyia kazi na anajua
tutafanya nini,”alisisiza Brandts ambaye kwa sasa anao wachezaji Mrundi
Didier Kavumbagu, Wanyarwanda Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite na Hamis
Kiiza wa Uganda, ambaye alikuwa dakika za mwisho kumalizana na Yanga,
hivyo kubakiwa na nafasi moja ya mchezaji wa kigeni.
Alipoulizwa kama atamkosa Oloya ni mchezaji wa
aina gani anayemuhitaji, Brandts alisema kwa sababu hajajiunga na timu
yoyote bado, hawezi kuzungumzia zaidi.
Kwa upande wa kambi ya Simba awali, Mwenyekiti
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe alisema wameshamalizana
na Oloya na wamemwacha uhuru yeye mwenyewe amalizane na Saigoni ili atue
Simba kabla ya msimu wa Ligi Kuu Bara kuanza.
Oloya mwenyewe alipozungumza na Mwanaspoti hivi
karibuni alisema kuwa mipango yake ilikuwa ni kwenda Simba na akakiri
kuwa amewahi kufanya mazungumzo na Yanga, lakini alikuwa amefika mbali
zaidi na klabu ya Msimbazi kimazungumzo.
Hata hivyo, wachezaji hubadilika kama kinyonga, na
ndio maana Mbuyu Twite alisaini mkataba wa Simba kabla ya kuruka
kimanga na kutua Jangwani, hivyo suala la Oloya ni jambo la kusubiri
mpaka dakika ya mwisho kujua atacheza Jangwani au Msimbazi.
Kocha wa Yanga ana historia katika ulimwengu wa
soka akiwa anacheza beki ya kati ya taifa lake la Uholanzi alifunga
mabao mawili kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1978 dhidi ya
Italia, alifunga na kujifunga katika mechi hiyo hivyo matokeo kuwa 1-1.
Katika hatua nyingine, Brandts amezungumzia kambi ya kikosi
chake na kusema anahitaji kambi nyingine ambayo atapata uwanja wenye
sehemu nzuri ya kuchezea iwe ndani au nje ya nchi.
Alisema pia katika ziara ya Kanda ya Ziwa amepata
mazoezi ya kutosha baada ya kucheza na Express wakatoa sare ya 1-1 kabla
ya kufungwa 2-1 na baadaye wakatoka suluhu na Rhino ya Tabora.
“Hakuna tatizo kwenye kikosi changu ingawa kwa
Tabora mazingira ya uwanja ndiyo hayakuwa mazuri,” alisema Brandts na
kusisitiza washambuliaji wake ni wazuri ingawa wanakosa umakini kwenye
kufunga.
Yanga haina mpango wa kuwachukua Kabange Twite na Yaw Berko katika usajili wa msimu huu, badala yake inataka straika
WAPINZANI WA USAIN BOLT WAKUTWA NA HATIA YA KUTUMIA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU
Wanariadha wawili kati ya wanariadha wenye kasi kubwa duniani Tyson Gay, kutoka Marekani na Asafa Powell wa Jamaica -- wamepatikana na kosa kutumia madawa ya kusisimua misuli.
Gay, ambaye ni mwanariadha wa pili kwa kuwa na kasi kubwa ya kukimbia katika mbio za mita mia moja, amesema anajiondoa kwenye mashindano ya dunia ya riadha yanayotarajiwa kufanyika mjini Moscow mwezi ujao.
Asafa Powell, ambaye alishikilia rekodi ya mbio za mita 100 hadi ilipovunjwa na Usain Bolt mwaka 2008, amekanusha kuwa alitumia dawa hizo makusudi.
Mwanariadha mwenzake wa Jamaica Sherone Simpson pia amepatikana na hatia ya kuzitumia dawa hizo za kusisimua misuli
EDINSON CAVANI ATUA PARIS KUFANYA VIPIMO VYA KUJIUNGA NA PSG
Sunday, July 14, 2013
THIAGO ALCANTARA AJIUNGA NA BAYERN MUNICH
Hatimaye kiungo wa kimataifa wa Spain na FC Barcelona Thiago Alcantara ameuzwa rasmi kwenda kujiunga na mabingwa wa ulaya na Ujerumani Bayern Munich.
Thiago ambaye alikuwa akihusishwa mno na kujiunga na Manchester United ingawa juzi kocha David Moyes alisema hawakuwahi kusema wanamhitaji mchezaji, amejiunga rasmi ya Bayern Munich kwa ada ya uhamisho wa 25 million euros.
Mapema wiki iliyopita kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola alikaririwa akisema kwamba anamhitaji Thiago kwenye timu yake na amewaomba viongozi wake kumsajili mchezaji huyo tu msimu huu.
Thiago amesaini mkataba wa miaka minne kuichezea Bayern Munich
STARS HAKIJAELEWEKA BADO CHANI

Wachezaji wa Taifa Stars wakiondoka katika uwanja wa Taifa , Dar es Salaam jana vichwa chini
Mfupa wa Waganda bado mgumu kwa Taifa Stars. Ni baada ya jana timu hiyo ya Tanzania kushindwa kufurukuta mbele ya wageni wao kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu kushiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) kufuatia kipigo cha bao 1-0.
Kwa matokeo hayo, Stars inahitaji miujiza kushinda
mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo kwenye uwanja ambao utaamuliwa
baadaye na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kati ya Namboole au
Nakivubo.
Katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Taifa
Stars ilitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza na kuwapa wakati
mgumu Uganda, lakini cha kusikitisha ni washambuliaji wake kukosa magoli
yasiyo na idadi.
Bao pekee la Uganda lilifungwa dakika ya 46
kupitia kwa Iguma Dennis aliyemfunga kipa Juma Kaseja kwa shuti la
pembeni ya lango akimaliza pasi ya shambulizi la kushtukiza kutoka kwa
Mpande Joseph.
Kwa matokeo hayo, Stars inaendelea kuwa mteja wa
The Cranes, na sasa ili isonge mbele itahitaji ushindi wa mabao 2-0
katika mechi ya marudiano.
Washambuliaji, John Bocco, Amri Kiemba, Mrisho
Ngassa waliinyima Stars mabao mengi ya hasa kipindi cha kwanza
walichotawala sehemu kubwa ya mchezo.
Uganda waliokuwa wakitumia nguvu nyingi kufika
lango la Stars, hawakupata nafasi nyingi za kufunga, lakini nafasi moja
waliyoipata ambayo haikuonekana kuwa ya hatari, ndiyo iliyowapa bao
pekee.
Stars walikuwa wa kwanza kupiga hodi lango la
Uganda dakika ya kwanza, baada ya krosi ya John Bocco kushindwa
kuunganishwa wavuni na Amri Kiemba aliyekuwa kiasi cha mita tano kutoka
langoni.Mrisho Ngassa aliyekuwa akiwakimbiza vizuri Waganda, alifanya
makosa kama ya Kiemba baada ya kushindwa kutikisa nyavu dakika ya 20
kufuatia pasi ya Bocco, ambaye naye dakika moja kabla alikosa bao la
wazi.
Taifa Stars waliendelea kuwanyong’onyesha
mashabiki wake baada ya kushindwa kufunga kupitia kwa Bocco katika
dakika 21 na 23, na baadaye dakika tatu Ngassa naye alikosa bao la wazi.
Shambulizi kubwa la The Cranes lilikuja dakika za
30 na 39, ambapo wangeweza kufunga mabao kama siyo nafasi hizo kupotezwa
na Edema Patrick.
Pamoja na Kocha wa Stars, Kim Poulsen kusema bado
kuna nafasi ya kushinda mchezo wa marudiano na kufuzu kwa michuano hiyo,
matumaini ni kidogo.
Akitetea wachezaji wake kupata nafasi nyingi na
kushindwa kufunga, Kim alisema: “Katika soka kukosa mabao ni jambo la
kawaida, bado tunaweza kushinda kwenye mchezo wa marudiano.” Kocha wa
Uganda, Sredojevic “Micho” Milutin alisema wachezaji wake walicheza kwa
kujituma na ndiyo maana wakapata ushindi ugenini.
SHIBOLI MOTO WA KUOTEA MBALI HUKO ZANZIBAR:
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba ya Dar es Salaam, Ali Shiboli ameisaidia
timu yake ya Jamhuri ya Pemba kupata pointi moja dhidi ya Bandari ya
Unguja.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Zanzibar uliochezwa juzi Alhamisi kwenye
Uwanja wa Gombani, Chakechake timu hizo zilifungana bao 1-1.
Shiboli hilo ni bao lake la tatu katika mechi tatu mfululizo ambazo
Jamhuri zimecheza katika ligi hiyo inayoelekea ukingoni.
Mshambualiji huyo alifunga mabao yake wakati Jamhuri ilipoichapa Malindi
mabao 3-1, ilipofungwa na KMKM mabao 3-2 na ilipotoka sare ya 1-1 na
Bandari.
Shiboli aliyeichezea Simba na baadaye kuuzwa kwa mkopo anaonyesha kuwa
amerejea katika kiwango chake kizuri cha kupachika mabao wavuni
kilichomfanya wakati fulani azigonganishe Simba na wapinzani wake wa
jadi, Yanga.
Timu zote hizo mbili zilipigania kumsajili mchezaji huyo baada ya
kuonyesha makali akiwa timu ya soka ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar
Heroes) na Simba ndiyo waliofanikiwa kunasa saini yake
MAN UNITED NJIANI KUMPOTEZA THIAGO ALCANTARA

Lakini sasa anaweza akabadili mawazo na kwenda kujiunga na kocha ambaye alimtambulisha kwenye soka la kimataifa wakati akiwa na Barca.
Guardiola alisema: “Namataka Thiago Alcantara. Nimewaambia Bayern wafanye kila kitu kumsajili lakini sijui nini kitatokea.
“Thiago ni mchezaji pekee ninayemhitaji, hilo ndilo nililowaambia.
“Nimsajili yeye au nisisajili kabisa. Tuna wachezaji wengi lakini tunahitaji ubora wa ziada ambao Thiago Alcantara atauleta.
“Namfahamu Thiago vizuri sana. Nimeongea na mwenyekiti Rummenigge na mkurugenzi wa ufundi Sammer kuhusu kumsajili, sasa tusubiri tuone nini kitatokea.
“Sidhani kuongeza kiungo mwingine kutaleta tatizo kwetu. Nimeongea na klabu kuhusu mpango/wazo wangu na sababu za kumhitaji Thiago.
“Nimewapa mawazo yangu, ;alini naisikiliza bodi itasemaje. Wakikataa pia ni sawa.”
MKUTANO TFF WAPITISHA MAREKEBISHO YA KATIBA
Mkutano
Mkuu Maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) uliofanyika leo
(Julai 13 mwaka huu) umepitisha marekebisho ya Katiba yake, hivyo
mchakato wa uchaguzi unatarajia kuanza wakati wowote.
Wajumbe
zaidi ya 100 walihudhuria Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa NSSF
Waterfron, Dar es Salaam na kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,
Joel Bendera aliyewataka wajumbe kuhakikisha kiwango cha mpira wa miguu
nchini kinakuwa.
Mkutano
huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga umefanya
marekebisho ya Katiba kutokana na maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA). James Johnson kutoka Idara ya Wanachama ndiye
aliyeiwakilisha FIFA katika mkutano huo.
Aprili
mwaka huu FIFA ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF, na kuagiza
kwanza yafanyike marekebisho ya Katiba ili kuingiza Kamati ya Maadili,
na Kamati ya Rufani ya Maadili ambavyo ndivyo watashughulikia matatizo
ya kimaadili kwa familia ya mpira wa miguu nchini.
Mbali
ya kamati hizo, mabadiliko hayo pia yametengeneza ngazi mbili za
kushughulikia masuala ya kinidhamu ambazo ni; Kamati ya Nidhamu na
Kamati ya Rufani ya Nidhamu.
Kamati
ya Utendaji ya TFF chini ya Rais Tenga itakutana kesho (Julai 14 mwaka
huu) kwa ajili ya kuteua wajumbe watakaounda Kamati hizo ili kuruhusu
kuanza mchakato wa uchaguzi ambao FIFA iliusimamisha hadi vitakapoundwa
vyombo hivyo.
KOCHA ANENA STRAIKA SIMBA NA BEKI YANGA
KOCHA Mkuu wa Rhino ya Tabora, Renatus Shija amezichambua Simba na Yanga, baada ya timu hizo za Dar es Salaam kucheza na timu hiyo katika mechi za kirafiki wiki iliyopita.
Simba iliifunga Rhino mabao 3-1 kabla ya timu hiyo ya Tabora kutoka suluhu na Yanga katika mchezo uliofuata.
Akizungumza na Mwanaspoti, Shija alisema:
“Washambuliaji wa Simba, ni wazuri mmoja mmoja, lakini wana uwezo
binafsi na wazuri kwenye umaliziaji kwani anapotafuta bao anapambana
mpaka mwisho kuhakikisha anafanikiwa.”
“Yanga wanao washambuliaji wengi wanaofahamika kwa
majina, wanacheza vizuri lakini hawana uwezo binafsi, mbinu za mmoja
mmoja katika umaliziaji hawana na wanapoteza nafasi nyingi za
mabao,”alisema Shija.
Simba walishinda mabao 3-1, mawili yakifungwa na Edward Christopher na Said Nassor ‘Cholo’.
Safu ya ushambuliaji ya Simba iliundwa na Msudani
Kun James, Betrem Momboki, Zahoro Pazi na Ramadhani Singano ‘Messi’
wakatoka na kuingia Ismail Rashid, Edward Christopher, Sino Agustino na
Marcel Kaheza.
Wakati Yanga ilikuwa na Mrundi Didier Kavumbagu,
Said Bahanuzi, Jerry Tegete akatoka akaingia Shaaban Kondo na Hamis
Thabit akatoka akaingia Abdallah Mguli.
“Kwa upande wa mabeki, Yanga ni wazuri sana,”
alisema Shija ambapo katika mchezo huo Yanga ilikuwa na Mnyarwanda Mbuyu
Twite, Rajab Zahir akatoka na kuingia Ibrahim Job pembeni kulikuwa na
Oscar Joshua na Juma Abdul licha ya kuwa mabeki wake mahiri wa kikosi
cha kwanza, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Devid Luhende
wapo na Taifa Stars.
Na Simba ilikuwa na Cholo, Samwel Ssenkoomi na
Asuman Buyinza akatoka akaingia Mussa Mudde wote raia wa Uganda, Omary
Salum akatoka akaingia, Haruna Shamte.
Shija alichambua pia kwenye kiungo na kukimwagia
sifa kikosi cha Msimbazi: “Simba ilikuwa nzuri kwenye kiungo zaidi ya
Yanga, wanacheza kwa ushirikiano katika kuzuia na kushambulia pia.”
Kiungo ya Simba ilichezwa na Jonas Mkude na Mcongomani Kuipou Felix wakati Yanga ni Salum Telela na Nizar Khalfan.
Hata hivyo huenda kiungo ya Yanga ilishindwa
kutamba kutokana na sehemu kubwa ya wachezaji wanaocheza nafasi hiyo
kama, Mnyarwanda Haruna Niyonzima kutokuwa na timu, Athuman Idd ‘Chuji’,
Frank Domayo na Simon Msuva wako na Taifa Stars.
MANCHESTER CITY YAPANDA DAU KWA RONALDO
MANCHESTER City imeanzisha vita mpya na majirani zao Manchester United baada ya kutangaza wameingia kwenye mbio za kumnasa mpachika mabao wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
Manchester City ipo tayari kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili staa huyo wa zamani wa Manchester United.
Mmiliki wa klabu sasa hataki mchezo na yupo tayari
kutoa dau kubwa iwezekanavyo na ameahidi kutoa mshahara wa pauni
300,000 kwa nyota huyo iwapo atakubali kutua Etihad.
Kwa miezi mitano, Manchester United imekuwa
ikijaribu kumshawishi mchezaji huyo mwenye miaka 28 bila ya mafanikio na
hawajakata tamaa, wanaendelea kumshawishi.
Man City wanafahamu kuwa vita hiyo ni kali lakini
wanaamini fedha ndiyo fimbo muhimu. Viongozi wa Manchester City
wanaishawishi Real Madrid imweke sokoni mchezaji huyo na kama wakikubali
jambo hilo, watatoa kiasi kikubwa cha fedha.
Mmiliki wa Man City, Sheikh Mansour amewaambia
viongozi wa juu wa klabu kuwa wanatakiwa kufanya kila liwezekanalo
kumnasa nyota huyo ili kushtua dunia.
Ronaldo amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake
na bado hajasaini mkataba mpya. Tayari viongozi wa Manchester City
wamewasiliana na wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes kwa ajili ya dili hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)