Pages

Tuesday, May 20, 2014

VAN GAAL AMTEUA VAN PERSIE KUWA NAHODHA MAN UNITED.

Double Dutch: Louis van Gaal (right) sees Robin van Persie as his perfect captain at Manchester United
 Waholanzi wawili: Louis van Gaal (kulia) anaona Robin van Persie ndiye nahodha aliyekamilika katika klabu ya Manchester United.
LOUIS van Gaal  anatarajia kumteua mshambuliaji wake hatari Robin van Persie kuwa nahodha wa kikosi chake mara atakapojiunga na Manchester United baada ya kumalizika kwa kombe la dunia majira ya kiangazi nchini Brazil.
Jumamosi iliyopita Van Persia aliifungia bao muhimu timu ya taifa ya Uholanzi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador na kulazmisha sare ya 1-1.
Van Gaal amekuwa na mahusiano mazuri na RVP ambaye ni nahodha wa timu ya taifa na sasa anatarajia kumpa jukumu hilo katika klabu ya Man United na kumpiga chini Rooney ambaye angekuwa nahodha wa kudumu katika utawala wa David Moyes.
A sign of things to come? Van Persie (right) poses with Kluivert (left), Louis van Gaal's assistant manager
Class: Holland captain van Persie scored a fantastic volley in their 1-1 draw with Ecuador on Saturday
  Van Persie alikuwa na majeruhi kwa muda wa wiki sita za mwishoni mwa msimu mbovu wa Man United baada ya kuumia goti katika mechi ya UEFA dhidi ya Olympiacos mwezi machi mwaka huu.
‘Hata kama ametokea katika majeruhi, alifunga bao la maajabu, bao ambalo huwezi kuamini, ni bao zuri mno,’ alisema  Van Gaal baada ya mshambuliaji huyo kusawazisha dakika ya 37 katika uwanja wa  Amsterdam ArenA jumamosi.
Kwa mujibu wa Van Gaal, kwa asimilia 100, Van Persie hayuko fiti lakini alionekana kuwa imara na kuitendea haki pasi ya Feyenoord na kufunga bao muhimu.
‘Nilifurahishwa na kiwango chake, pia ni nahodha wa aina yake,” Alisema Van Gaal. “Nadhani unampa mchezaji unahodha kama mna morali na falsafa inayofanana”.
“Sio tu mambo ya uwanjani na kiwango cha mchezaji, hata maisha ya kawaida tu”.
“Naamini hilo ni muhimu sana. Naamini Van Persie na Van Gaal tuna falsafa moja”.

Saturday, May 17, 2014

PUMA WAZINDUA NJUMU MPYA ZITAKAZOVALIWA NA BALOTELLI, FABREGAS KOMBE LA DUNIA

Puma Launch EvoPOWER World Cup Boots with Mario Balotelli, Cesc Fabregas
KAMPUNI ya kutengeneza vifaa vya michezo ya PUMA imezindua viatu vya EvoPOWER kwa ajili ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Viatu hivyo vimezinduliwa na wachezaji nyota wawili,  Mario Balotelli wa Italia na Cec Fabregas wa Hispania.
Viatu vya Puma
Wachezaji wa Arsenal wakitumia viatu vya Puma katika mazoezi
Daluga za Puma ni moyo mwingine
Cesc Fabregas akiwa katinga buti za Puma tayari kwa kazi

KLABU ZA ULAYA ZILIZOONGOZA KWA WACHEZAJI WENGI KWENDA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014.

Homeward bound: Brazil defender David Luiz is one of 18 Chelsea players in line to play at the World CupArdhi ya nyumbani: Beki wa Brazil ,  David Luiz ni miongoni mwa wachezaji  18 wa Chelsea wanaotarajia kushiriki kombe la dunia mwaka huu na nchi zao.
KLABU ya Chelsea ndio timu pekee ambayo wachezaji wake wengi wanaenda kushiriki fainal za kombe la dunia kuanzi mwezi ujao nchini Brazil.
 
Wachezaji 18 wa Chelsea wanatarajia kuzichezea nchi zao katika fainali hizo kubwa za soka duniani.
Ukiangalia vikosi vya awali vya mataifa mbalimbali na vikosi vya mwisho vya watu 23 , wachezaji wengi wa Chelsea wamechaguliwa, huku wakifuatiwa na Manchester United ambayo wachezaji wake 16 wamechaguliwa licha ya kuwa na msimu mbovu.
Kwa wenyeji Brazil, kocha Luiz Felipe Scolari amewaita Oscar, Willian, Ramires na  David Luiz kuichezea nchi yao katika ardhi ya nyumbani.
Still going strong: Chelsea midfielder Frank Lampard (right) has been included in England's 23-man squad
Bado ana nguvu: Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard (kulia) ametajwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya England
In the frame: Fernando Torres is hoping to be chosen in Spain's final list after a disappointing season for Jose Mourinho's side
Kama kawaida: Fernando Torres anatarajiwa kutajwa katika orodha ya mwisho ya kikosi ch Hispania licha ya kutokuwa na msimu mzuri chini ya Mourinho.

KLABU AMBAZO WACHEZAJI WAKE WENGIN WANAKWENDA KOMBE LA DUNIA

1. Chelsea (18)
2. Manchester United, Bayern Munich (16)
3. Napoli (14)
4. Barcelona, Real Madrid, Manchester City (13)
5. Juventus, Arsenal, Liverpool (12)
6. Atletico Madrid (11)
7. Porto, Inter Milan, AC Milan, Zenit (10)
8. Borussia Dortmund, Paris Saint-Germain (8)
9. Southampton, Schalke, Roma (7)
The Blues pia wachezaji wake wawili wa England, Frank Lampard na Gary Cahill, Wawili wa Hispania,  Fernando Torres na Cesar Azpilicueta na nyota wa Ubelgiji,  Eden Hazard, Romelu Lukaku na Thiabaut Courtois wameitwa katika vikosi vya nchi zao.
Wachezaji wengine waliobaki watacheza kombe la dunia na nchi zao. Samuel Eto`o ataichezea Camroon,  Ujerumani, Andre Schurrle, Nigeria,  John Obi Mikel, Victor Moses na Kenneth Omeuro, Ghana, Christian Atsu na Uholanzi,  Patrick van Aanholt.
Licha ya Man United kuvurunda zaidi msimu huu, lakini haijazuia wachezaji wake kuitwa vikosi vya timu za taifa.
Wayne Rooney, Javier Hernandez na Robin van Persie watacheza fainali za kombe la dunia, japokuwa wachezaji wawili wa klabu hiyo Tom Cleverley na Michael Carrick wote wapo katika orodha ya wachezaji wa akiba.

 
 
 
On the plane: Manchester United striker Wayne Rooney is battling to be fully fit for Brazil

 
Back in action: Red Devils forward Robin van Persie looks set to play for the club's next manager, Louis van Gaal, on Holland duty
Amerudi kazini: Mshambuliaji wa mashetani wekundu, Robin van Persie anatarajia kuichezea Uholanzi chini ya kocha  mtarajiwa wa Man United, Louis van Gaal, ambaye kwa sasa ana majukumu na timu ya taifa ya Uholanzi.

Man United imetoa wachezaji idadi sawa na mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich ambao kwa asimilia kubwa wanaunda kikosi cha Ujerumani.

Manuel Neuer, Jerome Boateng, Bastian Schweinsteiger, Toni Kross, Thomas Muller, Mario Gotze na  Philipp Lahm wote wameitwa katika kikosi cha awali cha Joachim Low  ambapo atachuja kupata kikosi cha mwisho cha wachezaji  23.
Miamba ya Serie A , Napoli ni klabu ya tatu ambayo wachezaji wake wengi watashiriki kombe la dunia. Wanandinga wake 14 wameitwa katika vikosi vya awali vya mataifa tofauti wakiwemo Valon Behrami, Blerim Dzemaili na Gokhan Inler
Klabu hiyo ya Italia ina wachezaji wengi kuliko miamba ya Hispania, Real Madrid na FC Barcelona, ambapo wote wana wachezaji 13 wakiwemo Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Idadi hiyo ni sawa na wachezaji wa mabingwa wa sasa wa Ligi kuu soka nchini England, Manchester City wakiwemo wachezaji watatu wa Argentina,  Sergio Aguero, Pablo Zabaleta na  Martin Demichelis.
Arsenal na Liverpool wanaweza kuwa na wachezaji 12 nchini Brazil, ingawa Lucas Leiva anaweza kubadili idadi baada ya kuongezwa katika kikosi cha akiba cha  Scolar mapema wiki hii.
Midfield general: Germany's Bastian Schweinsteiger is one of 16 Bayern Munich players to have been called up
Star man: Portugal's Cristiano Ronaldo is one of 13 Real Madrid players included in World Cup squads
Threat: Barcelona's Lionel Messi will lead the line for Argentina back in South America this summer
 Tishio: Nyota wa Barcelona,  Lionel Messi ataiongoza Argentina katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mabingwa wa Italia,  Juventus,  wachezaji wake 12 wametajwa katika vikosi vya timu za taifa wiki hii na wanaweza kujiona hawana bahati baada ya mshambuliaji wao hatari, Carlos Tevez kutemwa na kocha  Alejandro Sabella.
Vinara wa La Liga na wanafainali wa UEFA, Atletico Madrid wanafuatia kwa wachezaji wake 11  kuitwa wakiwemo watatu wa Hispania Diego Costa, Koke na Juanfran.
Klabu nyingeni ambazo wachezaji wake wengi wameitwa timu za taifa ni Porto, Inter Milan, AC Milan, Zenit St Petersburg (zote wachezaji), Borussia Dortmund (nane) and Southampton (saba).
Brazil bound: Southampton's Maya Yoshida (right) and Liverpool's Luis Suarez (left) are both set to play in this summer's World CupNgoma za Brazil: Nyota wa Southampton, Maya Yoshida (kulia) na wa Liverpool,  Luis Suarez (kushoto) wote watacheza fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu.

SUAREZ HANG`ATUKI LIVERPOOL, ADAI ANA FURAHA KUBWA ANFIELD.

 Mshambuliaji Luis Suarez amesema hana mpango wa kuondoka Liverpool licha ya kutakiwa na vigogo wa La Liga, Real Madrid na Barcelona
MSHAMBULIAJI Luis Suarez amesema anapenda maisha ndani ya Liverpool na hafikirii kuondoka Anfield.
Nyota huyo wa Uruguay amemaliza msimu vizuri akiwa na Wekundu hao wa Anfield  kwa kufunga mabao 31 na kutwaa tuzo za Mwanasoka Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) na ya Waandishi wa Habari za Soka.
Mafanikio hayo yanakuja baada ya kupitia msimu mgumu uliopita akifungiwa kwa kumng’ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic – akilazimisha kupita.
Sasa wakati tetesi za usajili zimeanza tena, Suarez, ambaye mapema wiki hii alikanusha kuwa na nia ya kuhamia klabu nyingine kubwa Ulaya, ameamua kuuheshimu mkataba aliosaini Desemba mwaka jana.
Happy: Suarez only signed his new contract earlier this season and says he loves the club
Rewarded: The Uruguayan won the PFA Player of the Year, with Eden Hazard winning Young Player of the Year
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye ameripotiwa kutakiwa na Real Madrid, ameiambia Sky Sports kwamba: “Nilisaini mkataba kwa sababu napapenda haps na nina furaha dana hapa. Ikiwa haunt furaha hapa huwezi kusaini mkataba wowote,”.
 
“Liverpool kwangu ni moja ya timu bora duniani, kwa sababu hakuna mtu haps katika chumba cha kubadilishia nguo anafikiri mimi no bora zaidi ya wengine na watu hapa ndani ya Melwood wanafanya kazi vizuri,”alisema.

MESSI AKUBALI KUMWAGA WINO BARCELONA, SASA AVUTA MKWANJA MREFU ZAIDI YA CR7.

LIONEL Messi amekubali kusaini mkataba mpya katika klabu yake ya Barcelona na kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani ambapo atakuwa anavuta mkwanja wa paundi milioni 16.3 kwa mwaka.
Baba yake, Jorge, amekutana na maofisa wa klabu Javier Faus na Antoni Rossich wiki iliyopita na kusaini mkataba wake wa 7 ndani ya klabu ya Barcelona.
Messi ambaye mwezi juni atafikisha miaka 27 baada ya kuongeza mkataba huo,  sasa atakaa Barcelona mpaka mwaka 2018.
He's staying: Lionel Messi has agreed to sign a new deal keeping him at Barcelona
 Ataendelea kuwepo: Lionel Messi amekubali kusaini mkataba mpya katika klabu ya Barcelona
Boost: Messi agreeing a new deal is the news the Barcelona fans had been waiting for

Wednesday, November 27, 2013

USAJILI DIRISHA DOGO KUFUNGWA DESEMBA 15 - KUANZIA MSIMU UJAO WACHEZAJI WA KIGENI MWISHO WA 3 KWA KILA TIMU

Wakati dirisha dogo la usajili linafungwa Desemba 15 mwaka huu, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunazikumbusha klabu zote kuheshimu kanuni na kuzingatia muda uliowekwa.
Pia tunakumbusha kuwa kupeleka mchezaji kwa mkopo katika klabu nyingine hakutoi nafasi ya kusajili mchezaji mpya. Kama klabu ilisaji wachezaji 30 maana yake ni kuwa haina nafasi ya kuongeza wachezaji.
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni (foreign players), tunakumbusha kuwa kuanzia msimu ujao 2014/2015 watakuwa watatu tu badala ya watano wa sasa.
Kuhusu usajili wa wachezaji kutoka nje mpaka sasa hakuna hata klabu moja imeshaingia kwenye TMS kuomba uhamisho. Itakapofika Desemba 15, system ya TMS itafunga.

KOMBE LA CHALLENJI: ZANZIBAR HEROES KUFUNGUA MICHUANO NA SUDAN YA KUSINI KESHO



Michuano mikongwe barani Afrika ya kombe la Challenge kwa nchi za ukanda wa Afrika ya mashariki na kati Cecafa inatarajiwa kuanza hapo kesho kwenye viwanja vya Nyayo jijini Nairobi na Machakos nchini Kenya, kwa jumla ya nchi kumi na mbili kuwania taji hilo.
Wenyeji Harambee starz ya Kenya, machampioni watetezi wa taji Uganda The Creans, Walya Antelope ya Ethiopia, Ocean boyz wa Somalia, Zanzibar Heroes ya Tanzania visiwani, Kilimanjaro starz ya Tanzania bara, Sudani ya kusini na ile ya Kaskazini, zinamenyanya.
Nyingine ni pamoja na Eritrea, Intamba Murugamba ya Burundi, Amavubi ya Rwanda, na waalikwa kwenye michuano hiyo Askari wa Chipolopolo toka nchini Zambia, zinawania taji hilo.
Timu zimegawanywa kwenye makundi ya A,B na C, ambapo kundi la A wapo Zanzibar Heroes ya Zanzibar, Walya Antelope ya Ethiopia, Sudan ya Kusini, na wenyeji Harambee starz ya Kenya, watasaka nafasi mbili za juu kucheza robo fainali.
Kundi la pili, lina timu za Kilimanjaro starz ya Tanzania bara, Chipolopolo ya Zambia, Intamba Murugamba ya Burundi, na mabaharia wa Somalia.
Kundi la tatu ambalo ni la C, lina timu za Amavubi ya Rwanda, machampioni watetezi wa taji Uganda the Creans, Sudan ya Kaskazini na mabaharia a Somalia.
Mechi za ufunguzi za michuano hiyo zinatarajiwa kuanza kesho kwa michezo baina ya wenyeji Harambee starz ya Kenya dhidi ya Walya Antelope ya Ethiopia kwenye uwanja wa Nyayo, lakini kabla utapigwa mchezo baina ya Zanzibar Heroes dhidi ya Sudani ya kusini.

Tuesday, November 26, 2013

JEZI MPYA ZA BRAZILI ZA KUCHEZEA KOMBE LA DUNIA 2014.





CHUJI, CANNAVARO, MSUVA NA JERRY TEGETE WAONGEZA MIKATABA YANGA - KUBAKI JANGWANI MPAKA 2016

Wachezaji watano wa timu ya Young Africans wameongeza mikataba ya muda mrefu ambapo sasa wataendelea kuitumikia klabu yenye maskani yake mitaa ya Twiga/Jangwani mpaka mwaka 2016, hili limefanywa na uongozi kwa mapendekezo ya benchi la ufundi.

Wachezaji ambao mpaka sasa wameshaongeza mikataba ya kuitumikia klabu ya Young Africans ni walinzi Kelvin Yondani (2014-2016), Nadir Haroub "Cannavaro" (2014-2016), kiungo Athuman Idd (2014-2016), mshambuliaji Saimon Msuva (2014-2016) na Jerson Tegete (2014-2016).

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb amesema hao ni baadhi tu ya wachezaji ambao wameshamaliza taratibu zote na kusaini mikataba mipya itakayowafanya waitumikie Yanga mpaka mwaka 2016.

"Tupo katika mazungumzo ya mwisho na wachezaji wetu wengine, mazungumzo yanaendelea vizuri na tunaamini muda si mrefu nao tutakua tumeshamalizana nao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga tena kwa muda mrefu "alisema Bin Kleb.

Wakati huo huo kikosi cha Young Africans leo kimeanza mazoezi asubuhi katika uwanja wa Bora - Mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo wa hisani dhidi ya Simba SC Disemba 14, 2013, mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.

SOURCE: YANGA WEBSITE

RONALDO AONGOZA KWENYE KUWANIA UCHEZAJI BORA WA DUNIA.

Thursday, November 14, 2013

FUTURE YOUNG TAIFA STARS YAICHAPA TAIFA STARS 1-0.

Mshambulia wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa (kulia) akichuana na mchezaji wa Future Young Taifa Stars, Kabanda katika mchezo kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Kiungo wa Taifa Stars, Athuma Idd "Chuji" akichuana na mchezaji wa Future Young Taifa Stars,Paul Nonga.
Beki wa Stars Erasto Nyoni (kushoto), akichuana na mshambuliaji wa Future Young Taifa Stars, Simon Msuva.
Erasto Nyoni akipimana ubavu na Simon Msuva.
Chuji akimtoka Paul Nonga.
Uniwezi bwana mdogo......Chuji akichuana na Paul Nonga wa Future Young Taifa Stars.
Makocha wakijadiliana jambo wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wakishuhudia mechi hiyo kupitia katika jengo la Machinga Complex.
Msuva akitoka baada ya kuumia.
Moja ya hekaheka.

KIM ATEUA 32 KUIKABILI KENYA.



Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
Wachezaji walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

RAISI WA BAYERN MUNICH AMWAGA CHOZI AKITANGAZA KUTENGENEZA FAIDA KUBWA ZAIDI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 113


Raisi wa Bayern Munich Uli Hoeness, anakabiriwa na kesi ya kukwepa kodi itakasomwa mwakani, jana alitokwa na machozi wakati akitangaza klabu yake kuvunja rekodi ya kuingiza mapato makubwa katika cha 113 years.
Katika mkutano wa mkuu wa klabu, Hoeness, ambaye alipokewa kwa shangwe, alishindwa kujizuia na kuanza kulia baada ya mabosi wenzie kumsifia kuiongoza vizuri timu hiyo na kupata mafanikio ya kushinda makombe matatu msimu uliopita. 
Hoeness, ambaye anashtakiwa kwa kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye fedha zake zilizopo katika moja ya benki huko Uswis.
 
Hoeness, amekuwa katika klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 40 kama mchezaji, kocha na saa raisi, alizungumzia matatizo yake ya kisheria, akisema kwamba alifanya makosa na kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye akaunti yake ya nje.
'Nilifanya makosa kutokulipa kodi katika uwekezaji kutoka nje. Sikuchukua mamilioni ya fedha na kuyatoa nje ya nchi," alisema Hoeness, baada ya kujifuta machozi.  'Nitapambana na matatizo.'
'Nina imani kubwa na utawala wa kisheria wa Bavarian.
'Ninatumaini kwamba story hii itakuwa na mwisho mzuri mpaka kufikia mwezi  March. Na kama mpaka wakati huo nitaruhusiwa kuendelea kuwa hapa naahidi kuitumikia klabu hii mpaka pumzi yangu ya mwisho.'

HUYU NDIO MCHEZAJI MWINGINE ALIYESAJILIWA NA YANGA BAADA YA KASEJA.


Monday, November 11, 2013

TUZO ZA MWANASOKA BORA WA TANZANIA: HARUNA NIYONZIMA AIBUKA KIDEDEA, AWABWAGA KIEMBA NA YONDANI.

Hii ndio ilikuwa kamati iliyoratibu tuzo hizo :Zamoyoni Mogella ( Mwenyekiti ), Kenny Mwaisabula ( Kaimu katibu ), na wajumbe Shaffih Dauda, Boniface Wambura,Edo Kumwembe na Doris Malyaga.

  Godfrey Nyange akimkabidhi tuzo mwaamuzi bora Oden Mbaga.
Ezekiel Kamwaga akipokea  tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa niaba ya Abdallah Kibadeni.
Zamoyoni Mogella akitoa tuzo ya bao la mwaka kwa mwakilishi wa Thomas Ulimwengu.

Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga kushoto akimkabidhi tuzo ya Ufungaji Bora mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast katika tuzo za gazeti la Mwanaspoti usiku wa jana ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.




Kiungo wa Simba Amri Kiemba akipokea tuzo ya 11 Bora





Niyonzima akikabidhiwa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka.
Haruna Niyonzima akikabidhiwa zawadi yake ya kuwa mwanasoka bora wa Tanzania




  Haruna Shamte ( kushoto ),Ramadhani Singano pamoja na mdau.


 
Joseph Kimwaga wa Azam Fc ndiye alichukua tuzo ya mwanasoka chipukizi.


Rais wa zamani wa SAFA,Kirsten Nematandani akimpatia tuzo Haruna Niyonzima ya mwanaoka bora wa kigeni wa mwaka.
Juma Nature Kibla akitumbuiza kwenye tuzo hizo


Rais wa heshima wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Said El Maamry akimkabidhi tuzo ya Mchezaji bora wa Tanzania anayecheza nje, mwakilishi wa mshindi wa tuzo hiyo, Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya DRC