Leo
Jumamosi tarehe 13, July: Tanzania itapambana na Uganda kwenye uwanja
wa taifa katika mchezo wa kugombea nafasi ya kushiriki kwenye michuano
ya mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza kwenye ligi za
ndani.
Uganda Cranes ilitua
Bongo wakitokea kwao siku ya alhamisi. Kikosi cha wachezaji 18 na
kufikia kwenye hotel ya Sapphire iliyopo katikati ya jiji la Dar es
salaam wakionekana kuwa kwenye hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa leo
katika dimba la uwanja wa taifa unaoweza kubeba mashabiki zaidi ya
55,000.
Uganda wanatarajiwa kuchezesha wachezaji wengi wapya kwenye hatua hii ya
kimataifa. Ukimuacha mlinzi Dennis Iguma na kiungo Wasswa Mawanda,
ambao walicheza dakika zote 90 kwenye mchezo wa kugombea kwenda Brazil
2014 dhidi ya Liberia na Angola, wachezaji wote waliobakia bado
hawajaonja utamu wa soka la kimatiafa.
Hakuna beki wa kushoto asilia kwenye kikosi hiki cha Micho, ukizingatia
mchezaji aliyeitwa kuja kucheza kwenye nafasi hiyo Habib Kavuma,
aliondolewa kikosini baada ya kugundulika kwamba alipewa kadi nyekundu
kwenye mchezo wa 2011 CHAN dhidi ya Gabon. Hili linamuacha Micho
Akibakiwa na mbadala Yusuf Mukisa, beki wa kulia ambaye hujaribu kucheza
nafasi hiyo pia.
Wachezaji wengine ambao wana uzoefu kidogo na michuano ya CHAN ni Ayubu
Kisaliita, Patrick Edema, Tonny Odur Hamuza Muwonge, ambao walicheza
kwenye michuano ya CHAN iliyofanyika Khartoum, Sudan.
Kutokana kuwa ugenini - Micho anategemewa kuipanga timu yake huku
akicheza mchezo wa kuzuia sana na kushambulia kwa kushtukiza. Uganda
wanaweza kuanza kwa mfumo wa 4-2-1-3, baadae wakibadilika kuja 4-3-3 na
4-4-2 kadri muda unavyozidi kusogea.
MCHEZAJI WA KUCHUNGWA: Dennis Iguma
Dennis
Iguma ameimarika sana kwenye kiwango chake, kujiamini kwake na namna
anavyojua kucheza kitimu. Mchezaji huyu ambaye alitumia utoto wake
kupata mafundisho ya soka kupita chuo cha soka cha Entebbe, anaweza
kucheza popote uwanjani kwa kiwango kile kile anachocheza kwenye nafasi
yake ya kawaida.
Iguma, kwa sasa anaichezea klabu ya Sports Club Victoria University
anategemewa kuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Stars wakiongozwa na
Canavaro na Yondani.
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemrudisha kikosini beki wa kulia wa
Yanga, David Luhende akitoa picha kwamba Shomary Kapombe beki halisi wa
kulia atahamia upande wa kushoto. Hii inakuja baada kumpa mapumziko
Nyoni ambaye alicheza ovyo kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia dhidi
ya Morocco na Ivory Coast.
Huku Uganda ikiwa ndio timu iliyo juu kisoka kwenye ukanda wa Afrika
Mashariki, kocha wa Tanzania alizungumza na kusema yafuatayo."Utakuwa
mchezo mgumu sana kwetu kwa sababu Uganda ni timu nzuri; tumekuwa
hatuchezi vizuri sana dhidi yao katika mechi za hivi karibuni."
Wakiwaondoa washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu, ambao
wanacheza TP Mazembe ya DR Congo, Taifa Stars itakuwa na wachezaji saba
ambao walicheza kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia 2014.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Simba amekuwa na kiwango kizuri sana kuanzia
msimu uliopita kwa Timu yake ya klabu na sasa kwenye timu ya taifa. Ana
akili ya mpira, anatuliza mashambulizi na kupeleka mashambulizi kwa
adui pamoja kuwatengenezea nafasi wenzie. Ikiwa atacheza kwenye kiwango
chake cha juu basi Uganda watapata taabu sana kumchunga Kiemba asiweze
kuwadhuru.
TIMU ZINAZOWEZA KUANZA
CRANES XI (4-2-1-3):
Hamuza Muwonge (GK)
Nicolas Wadada - Savio Kabugo - Richard Kasagga - Yusuf Mukisa
Hassan Wasswa (Captain) -Dennis Iguma
Joseph Mpande
Tonny Odur -Patrick Edema - Ronald Muganga
TANZANIA XI (4-3-3)
Juma Kaseja (GK)- Captain
Shomari Kapombe - Yondan - Nadir 'Canavaro' Haroub - David Luhende
Sure Boy - Frank Domayo
Mwinyi Kazimoto
Mrisho Ngassa-John Bocco - Amri Kiemba
JE WAJUA ?
- Mpaka kufikia 12th July 2013, Uganda inashika nafasi ya 80 katika
listi ya timu bora duniani ya FIFA - wakati Tanzania ikishika nafasi ya
121 na pointi 271.
- Uganda Cranes ilifuzu kucheza 2011 CHAN Championships jijini Khartoum, Sudan kufuatia kuifunga Tanzania nyumbani na ugenini.
- Uganda ilifunga goli moja katika CHAN iliyopita iliyofanyika Sudan.
Ibrahim Saddam Juma alifunga goli dakika ya 77 dhidi ya Gabon.
-
Kocha wa Uganda, atakuwa anaiongoza UG kwa mara ya nne tangu amrithi
Bobby, ameshacheza dhidi ya Libya katika mechi ya kirafiki na kufungwa
3-0, akaja kushinda 1-0 na 2-1 dhidi ya Liberia na Angola katika mechi
za kufuzu kombe la dunia 2014.
Tanzania iliwahi kushirikia michuano hii wakati tu ilipoanzishwa na kufanyika nchini Ivory Coast
No comments:
Post a Comment