Pages

Friday, July 12, 2013

HAWA NDIO MAKOCHA 10 BORA DUNIANI

 
 

KUNG’ATUKA kwa Sir Alex Ferguson kumeacha vita kubwa kwenye soka juu ya ushindani wa makocha kwamba nani atakuwa bora kwa nyakati zote baada ya Mskochi huyo kuwahi kupachikwa cheo cha ‘Kocha Bora wa Dunia’.
Waswahili wanasema ‘Kila palipo na mwanamume mwenye mafanikio, nyuma yake kuna mwanamke bora’, hata katika soka ni hivyo hivyo kwamba, kila kwenye timu yenye mafanikio, nyuma yake kuna kocha bora.
Mfano ni Manchester City. Ilikuwa na kila kitu, mabeki wazuri, viungo mahiri na washambuliaji hatari, lakini haikuwa chini ya mikono ya kocha bora msimu uliopita ilijikuta ikitopoteza taji lake la Ligi Kuu England kwa timu iliyosaidiwa na kocha bora. Makala hii inaorodhesha makocha 10 bora wanaoendelea na kazi yao kwa sasa, wakipangwa si kwa mafanikio yao ya jumla, ingawa yamechukua nafasi yake.
10. Jurgen Klopp (Borussia Dortmund)
Kocha huyo ameingia kwenye orodha hiyo kutokana na namna alivyoijenga Borussia Dortmund kutoka kwenye timu isiyokuwa na nguvu sana kwenye ligi, hadi kuwa washindani wakubwa kwenye Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ na Ulaya, licha ya kwamba hakuweza kudumu kwa muda mrefu katika kikosi hicho.
Ubora wa Klopp, si tu kwa kile alichofanikiwa kukipata, lakini ni kile anachokitarajia kukipata kutokana na namna alivyouinda timu yake. Kikosi chake cha Borussia Dortmund kiliipoka Bayern Munich ubingwa wa Bundesliga na hakuishia kulitwaa tu taji hilo mara mbili mfululizo, bali kuweka rekodi ya pointi kwenye ligi hiyo, huku akitwaa ubingwa wa Kombe la Ligi bila ya kufanya usajili mkubwa.
Kwa sasa pamoja na Bayern Munich kumnasa nyota wake, Mario Gotze na Shinji Kagawa aliyehamia Manchester United mwaka jana, huku Robert Lewandowski naye akiwindwa vikali na timu nyingine, kwa Dortmund si tatizo kama Klopp ataendelea kubaki.
9. Guus Hiddink (Anzhi)
Kujulikana kwa ubora wake kumetokana na kuzinoa timu za taifa, lakini alifanikiwa kwenye klabu.
Akiwa na PSV Eindhoven, alitwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie) kati ya mwaka 1987 na 1989 na alirudia mafanikio hayo katika miaka ya 2003, 2005 na 2006.
Alihamia kwenye soka la kimataifa na pamoja na kwamba hakuweza kutwaa chochote huko, lakini namna alivyoweza kuzibadili timu ndogo na kuwa tishio hilo linatosha kuthaminisha ubora aliokuwa nao.
Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002 alikuwa na kikosi cha Korea Kusini na kuifikisha nusu fainali timu hiyo kabla ya kufungwa na Ujerumani. Miaka minne baadaye alihamia Australia na kuifanya timu hiyo kuwa tishio kwenye Kombe la Dunia 2006 lililofanyika Ujerumani kwa kuishia raundi ya pili.
Miaka miwili baadaye alikuwa na kikosi cha Urusi na kukifikisha nusu fainali ya Euro 2008, hapo wakifanikiwa kuwatupa nje Uholanzi na waliokuwa mabingwa watetezi, Ugiriki kabla ya kutupwa nje na waliokuwa mabingwa, Hispania. Kwa sasa yupo na kikosi cha Anzhi.
8. Arsene Wenger (Arsenal)
Ameporomoka kidogo tangu zama zile za Arsenal isiyoshindika, lakini kikosi chake kwa misimu minne mfululizo kimepiku hatari ya kupitwa na mahasimu wao, Tottenham Hotspur katika msimu wa Ligi Kuu England.
Baadhi ya mashabiki wanaonekana kuchoshwa na hali ya Arsenal ya sasa kutokana na kushindwa kuonyesha upinzani, jambo ambalo linawatisha na kuhofia kuwa kama kilichotokea Liverpool.
Lakini, ukweli halisi, kulingana na sera za timu hiyo, uwepo wa Wenger utaisaidia kuendelea kuwapo kwenye nafasi za juu.
Timu hiyo imekuwa na bajeti isiyoridhisha kwenye usajili, lakini kwa kulinasa jina kubwa la Gonzalo Higuain , Wenger anaweza kurejesha makali kwenye timu hiyo kama ilivyokuwa mwaka 1996 alipowasili klabuni hapo.
7. Rafael Benitez (Napoli)
Rafa inaweza kuonekana kama asingeingia kwenye orodha hii baada ya kile kilichotokea Chelsea.
Lakini kutwaa ubingwa wa Ligi ya Europa lililokuwa taji la pili la Ulaya kwa klabu hiyo ndani ya miaka miwili, hilo limempandisha chati tangu alipoharibu kwenye nyakati zake pale Inter Milan.
Kwa ujumla, Rafa amekuwa kocha mwenye mafanikio, akiweza kuzipandisha Extremadura na Tenerife kucheza La Liga kutoka daraja la pili, kabla ya kutwaa mataji mawili ya La Liga akiwa na kikosi cha Valencia, ambapo alivunja utawala wa timu za Real Madrid na Barcelona zilizokuwa zikipokezana ubingwa.
Baadaye akahamia Liverpool na kuleta mapinduzi makubwa. Akahama Liverpool na kutimkia Inter Milan, mahali ambako alikwenda kutwaa Klabu Bingwa ya Dunia, lakini alifanya hivyo akiwa na timu iliyotengenezwa na Jose Mourinho.
Alirejea England na kujiunga na Chelsea, Rafa alikumbana na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki, akawapa taji la Europa League kabla ya msimu ujao kuonekana katika benchi la Napoli ya Italia.
6. Vicente Del Bosque (Hispania)
Ingawa ubora wa Del Bosque unatazamwa kwa Hispania inavyocheza soka lake la kuvutia tangu alipochaguliwa kukinoa kikosi hicho mwaka 2008, ameng’ara akiwa na msitu wa wachezaji mahiri kabisa duniani. Lakini umahiri wa Del Bosque haukuanza kuonekana sasa, ilikuwa hivyo tangu alipokuwa Real Madrid kati ya mwaka 1999 na 2003 ambapo alitwaa mataji mawili ya La Liga, moja la ligi na mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na jingine la Super Cup.
Hivyo ni wazi kabisa huyo ni kocha bora kabisa licha ya kwamba hakuwahi kulithibitisha hilo akiwa na kikosi chenye bajeti ndogo kwenye usajili au timu yenye kiwango cha chini.
5. Pep Guardiola (Bayern Munich)
Jina lake limepata kuwa kubwa baada ya kile alichokifanya Barcelona, hakika Guardiola ameliteka soka la dunia kwa staili ya aina yake. Akitumia mwaka mmoja tu kwenye kikosi cha Barcelona B, kocha huyo alipelekwa kikosi cha kwanza na tangu hapo hakurudi nyuma.
Alibaki na kikosi hicho kutoka mwaka 2008 hadi 2012, ndani ya miaka hiyo minne, ameweza kutwaa mataji matatu ya La Liga, matano ya Copa del Rey, mawili ya Ligi ya Mabingwa, mawili ya Super Cup na mawili ya Klabu Bingwa ya Dunia.
Ubora wake haupo kwenye kutwaa mataji pekee, bali namna alivyoweza kuifanya Barcelona kucheza soka la gonga za pasi nyingi na ‘tiki-taka’, mfumo ambao umehamia pia kwenye timu ya taifa na kuweza kuteka dunia.
Guardiola, 42, aliondoka Barcelona mwaka jana na mwaka huu alitangazwa kuinoa Bayern Munich.
4. Carlo Ancelotti (Real Madrid)
Ancelotti bado anasugua kichwa kujiweka sawa baada ya kile kilichomkuta Chelsea, mahali ambapo aliondolewa na Roman Abramovich miaka miwili iliyopita.
Lakini, hilo si la kusumbuka sawa, kwani hata Roberto Di Matteo aliyefika kwenye timu hiyo na kuipa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, naye amefunguliwa mlango wa kutokea na hakudumu kabisa.
Mwaka huu, ameamua kuondoka PSG na atakuwa mrithi wa Jose Mourinho katika kikosi cha Real Madrid. Ancelotti ni kocha mwenye hadhi kubwa, kwa kipindi cha miaka minane aliyokuwa na kikosi cha AC Milan, amenyakua kila aina ya mataji kwenye kikosi hicho na kuliweka jina lake juu.
Alipokwenda Chelsea, aliisaidia timu hiyo kunyakuwa mataji mawili kwa msimu mmoja ikiwa ni mara yao ya kwanza, lakini mwaka uliofuata wakapigwa kikumbo na Manchester United kabla ya kuondolewa na Roman Abramovich.
3. Louis Van Gaal (Uholanzi)
Hii ni mara yake ya pili kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, lakini ni jambo linalotia masikitiko kwamba mafanikio yake makubwa kocha huyo ni kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Ajax mwaka 1995.
Miaka yake aliyokuwa na kikosi hicho cha Ajax, Van Gaal, aliweza kutwaa mataji kadha, ikiwamo mataji matatu mfululizo ya ligi, taji la Uefa Cup na Super Cup.
Lakini, tangu alipotwaa ubingwa wa Ulaya, maisha ya soka la Van Gaal yamepita kwenye nyakati nyingi tofauti, alihamia Barcelona na kuipa mataji mawili ya La Liga, kisha akatua Bayern Munich na kuipa Bundesliga na baadaye alirejea Uholanzi kuinoa AZ Alkmaar na kuwapa ubingwa wa Eredivisie mwaka 2009.
2. Ottmar Hitzfeld (Uswisi)
Kumtaja Ottmar Hitzfeld kwenye orodha hii kunaweza kuonekana kama masihara kutokana na umri wake, lakini ukweli bosi huyo atabaki kuwa wa daraja la juu baada ya kile alichokifanya Ujerumani na Uswisi, ikiwamo ya kutwaa mataji mawili ya Ulaya katika klabu mbili tofauti.
Aliaza kuipa mafanikio Grasshoppers ya Uswisi kwa kunyakua mataji mawili ya mfululizo ya ligi na kisha baadaye kuhamia Borussia Dortmund mwaka 1991.
Ilimchukua Hitzfeld misimu minne tu kunyakua Bundesliga mwaka 1995 na 1996, wakati huo katika miaka hiyo akitwaa German Supercup na baadaye akaipa Dortmund ubingwa wake wa kwanza wa Ulaya mwaka 1997.
Baadaye akahamia Bayern na akaendeleza makali yake, kabla ya mkataba wake kufika mwisho 2004, alitwaa mataji manne ya Bundesliga mfululizo, ikiwamo kutwaa mataji mawili kwa msimu mmoja mara mbili, kisha akaipa taji la Mabingwa Ulaya na kuondoka hapo akiachana alama zake.
Baadaye Bayern Munich ilimsainisha mkataba mwingine, ambapo kwenye msimu wake wa mwisho wa 2007-08, aliipa ubingwa wa ligi kabla ya kuhamia timu ya taifa ya Uswisi.
1. Jose Mourinho (Chelsea)
Alipowasili Real Madrid mwaka 2010, Dunia ilitambua itaona upinzani mkali katika historia ya soka Hispania baada ya kuwapo Guardiola katika kikosi cha Barcelona.
Mourinho akabadili kila kitu, akamsumbua Guardiola na utawala wake katika La Liga, kabla ya Mhispania huyo kuamua kuachia ngazi.
Ndani ya uwanja wa soka, Mourinho ni mmoja wa makocha wenye mafanikio, alitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, akifanya hivyo na FC Porto mwaka 2004 na kisha kurudia akiwa na Inter Milan mwaka 2010.
Alipohamia Chelsea, Mourinho alijipachika jina la ‘Special One’ na hapo akaweza kuipa timu hiyo ubingwa wa Ligi Kuu England miaka miwili mfululizo baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka 50 kabla ya kutimkia Inter Milan ya Italia.
Sasa amerejea Stamford Bridge akitokea Real Madrid, huku kurejea kwake kwa safari hii kukikabiliwa na mtihani mkubwa wa kufanikisha kile alichoshindwa kukifanya wakati ule, kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kucheza soka la kuvutia.

THAMANI YA IBRAHIMOVIC NA RONALDO ZATIKISA ULAYA KWENYE USAJILI

 Ibrahimovic 

USAJILI wa wanasoka barani Ulaya umeanza kupamba moto, tumeanza kuona nyota kadhaa wakinaswa.
Wiki hii tumemshuhudia Neymar akinaswa kutoka Santos kwenda Barcelona kwa ada ya Euro 57 milioni, naye Jesuz Navas alihama kutoka Sevilla kwenda Manchester City kwa Pauni 17 milioni.
Huo ni mwanzo tu, huenda tukashuhudia usajili wa fedha nyingi zaidi, lakini je ni nani anayeongoza kwa kusajiliwa kwa fedha nyingi katika historia ya soka? Jibu ni Zlatan Ibrahimovic.
Mchezaji huyo kutoka Sweden ndiye kinara wa fedha nyingi na amehama kwenye klabu saba tangu mwaka 2002 na kufanya jumla ya usajili wake kuwa wa Euro 169.1 milioni.
Ibrahimovic alijiunga na PSG akitokea AC Milan katika dirisha la usajili la msimu uliiopita kwa Euro 23 milioni na hapo ndipo alitimiza klabu saba tangu alipoanza kuhama.
Mchezaji huyo alianza kwa kuondoka Malmo FF kwenda Ajax kwa ada ya Euro 9 milioni mwaka 2002, Juventus ililipa Euro 16 kwa klabu ya Ajax ili kumnasa mwaka 2004, nayo Inter Milan ilimnunua nyota huyo kutoka Juventus kwa Euro 24.8 milion (2006).
Baadaye Barcelona ilimnunua kwa Euro 69.5 milioni kutoka Inter Milan (2009). Usajili huo ulishika namba tatu katika historia ya fedha za usajili duniani. 
Mwaka 2011 aliondoka Barcelona kwenda AC Milan kwa Euro 27 milioni. Lakini Cristiano Ronaldo, aliyehama mara mbili tu kwenye maisha yake ya soka, anashika nafasi ya tano na amesajiliwa kwa jumla ya Euro 111.5 milioni.
Mchezaji huyo alitoka Sporting Lisbon kwenda Man United kisha akaondoka Old Trafford kwenda Real Madrid kwa Euro 94 milioni ukiwa ni usajili mkubwa zaidi kwa mara moja kuwahi kutokea duniani.
Nyota wa Ireland, Robbie Keane, ndiye mchezaji ambaye amehama klabu nyingi zaidi tangu mwaka 1999 ambapo ameibuka kwenye klabu tisa.

JUMA KASEJA KUWA MRITHI WA CASSILAS MTIBWA SUGAR


ENDAPO Mtibwa Sugar ya Morogoro itamuuza kipa wake namba moja, Hussein Shariff ‘Casillas’ kwa FC Lupopo ya Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Congo imepanga kumsajili Juma Kaseja ambaye amemaliza mkataba wake na Simba.
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime alisema Casillas amefuzu Lupopo na kinachofanyika sasa ni makubaliano ya dau.
 “Iwapo tutamuuza Casillas, tutamsajili kipa mwingine bora kama Juma Kaseja ili kuhakikisha tunabaki katika hali nzuri na kumudu vyema mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.”
Mwezi uliopita, Hussein Sharif alinyakua tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka  ya Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza) na kuwafunika makipa wa Taifa Stars, Juma Kaseja na Mwadini Ali. Shariff atakuwa anatoka nje ya nchi kwa mara ya pili kwenda kucheza soka la kulipwa baada ya awali kushiriki Ligi Kuu Msumbiji mwaka 2008.
Wakati huohuo, kocha wa timu hiyo na pia nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Maxime alisema Mtibwa inazingoja klabu za Simba na Yanga kumaliza fujo za usajili na ndipo wao waanze.
Katika hatua nyingine, Coastal Union ya Tanga imekana kufanya mazungumzo ya usajili na Kaseja.
Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo ya Tanga, Nassor Binslum alisema klabu hiyo kuwasajili wachezaji wenye majina kama Haruna Moshi ‘Boban’ na Juma Nyoso haina maana kuwa ndio wamsajili Kaseja.
 “Tunatambua kuwa Kaseja ni kipa mzuri sana, lakini hana nafasi Coastal, usajili wa kina Boban ulifanyika kwa sababu tuliwahitaji kutokana na kupungukiwa na wachezaji na si kwa sababu

WENGER SAHANI MOJA NA MSHAMBULIAJI WA MANCHESTER UNITED

wayne.rooney.jpg

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger sasa ana kila sababu ya kutabasamu, hiyo ni kwa sababu ana uhakika wa kupewa pauni 70 milioni za usajili kila msimu. Jambo hilo linamaanisha kuwa klabu sasa itashindana na wakongwe wengine kwenye soka na wana uwezo wa kumnasa Wayne Rooney. Mkurugenzi Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis alisema Arsenal inaweza kulipa ada ya pauni 25 milioni na kumnasa Rooney ikiwa ni pamoja na kumpa mshahara wa pauni 200,000.
Gazidis alisema uamuzi wakumfuata au kutomfuata Rooney sasa upo mikononi mwa Wenger. Kiongozi huyo alisema anaamini fedha hizo zitatosha kuifanya Arsenal isake ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao. 
 Habari zinasema kuwa Arsenal itapata fedha karibu pauni 300 milioni kutoka katika mapato mbalimbali na watakuwa na uwezo wa kutoa pauni 70 milioni za usajili kila mwaka.
 Ongezeko hilo la fedha ni furaha kwa mashabiki wa Arsenal ambao wamekuwa wakisubiri vikombe kwa muda mrefu. Arsenal nusura ishindwe kutua kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushikana mashati na Tottenham mpaka siku ya mwisho. Ushindi wao dhidi ya Newcastle ndio uliwafanya watue kwenye michuano hiyo mikubwa ya Ulaya.

DILI KUBWA : Rooney,Ronaldo kubadilisha jezi Man United

 

USAJILI umekolea, shughuli ‘inayobamba’ ni juu ya kuondoka au kutokuondoka kwa Wayne Rooney katika klabu ya Manchester United. Mchezaji huyo anayesakwa na Arsenal na Chelsea, amezua habari mpya! Yupo mbioni kubadilishana makao na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid. Habari kutoka Real Madrid zinasema kocha mpya Carlo Ancelotti anataka kumnasa Rooney ambaye amekuwa ‘akimzimia’ kwa muda mrefu na yupo tayari kumbadilisha na Ronaldo.
Imefahamika kuwa Real Madrid ipo tayari kumtoa Ronaldo kwa pauni 60 milioni na kwa kuwa Rooney ana thamani ya pauni 30 milioni, Manchester United itakuwa na kazi rahisi ya kulipa pauni 30 milioni tu kukamilisha mpango huo.
Kocha mpya wa Manchester United, David Moyes anatarajiwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana mchezaji wake wa zamani wa Everton (Rooney) ili afahamu msimamo wake wa mwisho.
Moyes anatamani Rooney abaki Old Trafford na kuanza upya baada ya mchezaji huyo kukorofishana na kocha wake wa zamani Alex Ferguson. Lakini kama Rooney mwenye miaka 27 akisema anataka kuondoka, Moyes hawezi kumzuia. Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa klabu za England zilizo mstari wa mbele kutaka kumsajili mchezaji huyo lakini ukweli ni kwamba mchezaji huyo anaweza kutua Real Madrid ambapo ameahidiwa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki.
Habari kutoka Manchester United zinasema kuwa duka la vifaa vya michezo la klabu limeanza kuchapisha jezi  namba ‘7’ ambayo alikuwa ikivaliwa na Ronaldo.

MASTAA MGUU NJE MGUU NDANI UINGEREZA

 
 

PILIKA PILIKA za usajili zinaendelea. Kuna wachezaji ambao wanakaribia kunaswa na kuna wengine hawana dalili yoyote.
Wachezaji wa aina hiyo huishia kutajwa tu. Makala hii inachambua mastaa ambao wanakaribia kutua au kutimka katika siku za karibuni.
 Henrikh Mkhitarayan (Shakhtar Donetsk kwenda Liverpool)
Liverpool imekuwa ikimsaka mchezaji huyo kwa muda mrefu na kuna kila dalili kuwa Mkhitarayan mwenye umri wa miaka 24 atatua kwenye kikosi cha Anfield.
Tetesi zilizopo ni kuwa Luis Suarez anakaribia kwenda Real Madrid, jambo hilo linawanyima usingizi viongozi wa Liverpool ambao wameapa kumsajili.
Mchezaji huyo amefunga mabao 42 kwenye mechi 103 katika kikosi chake cha huko Ukraine.
Makubaliano ya usajili wa Pauni 22 milioni yamefanyika na kwa kuwa Liverpool imemuuza Andy Carroll kwenda West Ham United, ina fedha za kutosha kumsajili mchezaji huyo.
Tottenham na Borussia Dortmund nazo zinamwania. Wiki iliyopita, mchezaji huyo hakufanya mazoezi na klabu yake kufuatia madai kuwa anaweza kuondoka haraka.
David Villa (Barcelona kwenda Spurs)
Tottenham imekuwa ikipigana vikumbo na majirani zake Arsenal katika jitihada za kusaka saini za wachezaji, lakini huenda ikaipiku kwa kumsajili David Villa.
Villa amekosa namba kwenye kikosi chake baada ya kupona maumivu ya mguu, sasa anataka kuondoka. Kuwasili kwa Neymar akitokea Santos kunafanya mchezaji huyo atafute mlango wa kutokea

MJUE MFADHILI MPYA WA CLUB YA SIMBA, BILIONEA WA KITANZANIA ANAYETAKA KULETA USHINDANI WA KIMAENDELEO NA MANJI!



RAHMA Al Kharusi si jina geni katika mchezo wa soka Tanzania, wengi wanamkumbuka wakati alipoamua kuingia katika kuisaidia Twiga Stars na baadaye akaipeleka nchini Marekani lakini baadaye akapotea.
Akarejea akiwa upande wa African Lyon, akasaidia mambo mengi na kufanya timu hiyo izidi kupata umaarufu, lakini baadaye hakuonekana hadi alipokuja kuibukia Simba na kusema hapo ndiyo nyumbani.
Mfanyabiashara huyo bilionea anasisitiza ametua Simba baada ya kuombwa kukubali uteuzi wa mjumbe wa kamati ya utendaji na anaamini atakuwa mshindani mkubwa wa kuleta maendeleo.
Rahma ni Rais wa Makampuni ya RBP Oil ambayo yanafanya biashara mbalimbali katika nchi tofauti za Afrika. Baadhi ya biashara hizo ni uuzaji wa mafuta ya ‘dizeli’ na petrol katika nchi mbalimbali, lakini pia vyakula pamoja na samani za ndani.
Nchi za Afrika ambazo makampuni yake yanafanya kazi ni pamoja na Tanzania, DR Congo, Sudan Kusini na Uganda lakini pia kampuni zake zinafanya biashara katika nchi za Oman na Qatar.
Rahma, maarufu kama Queen of Bees, yaani Malkia wa Nyuki, anataka Simba yenye mabadiliko makubwa huku akitumia msemo wa, “Nikianza jambo, lazima nilimalize.”
Anataka kuiona Simba ikiwa na mambo mengi yenye mabadiliko, lakini anataka timu ya wanawake pamoja na timu imara ya vijana ambayo itaiwezesha Simba kuwa na msingi hapo baadaye.
“Simba walikuja kuniomba, sikuona kama kuna ubaya wa kukubali kuingia. Wakati tunakua nyumbani nilikuwa nikimuona baba yangu akiisaidia Simba, nasi tukajikuta tunaingia Simba. Tangu nikiwa mdogo, hii ndiyo timu yangu.
“Huo ni ushabiki, lakini ninachotaka mimi ni maendeleo. Najua kuna presha kubwa kutoka kwa Yanga, mimi nitaichukulia kama changamoto na nitashindana kuleta maendeleo. Najua Yanga wanaye (Yusuf) Manji, nitashindana naye sana.
“Najua nikishindana na Manji nitaleta maendeleo upande wa Simba, lakini nitapenda uwe ushindani wa kimaendeleo na si zaidi. Kama nitaona ni ushindani wa kutaka kuumizana nitajiweka kando, nataka maendeleo ambayo ndiyo mafanikio.
“Sitaki ugomvi, ndiyo maana utaona nilijiondoa Twiga na African Lyon. Migogoro ni kati ya vitu nisivyopenda kabisa, halafu Manji ni mtu ninayeheshimiana naye sana. Hivyo sitaki malumbano ila ushindani wa kuleta maendeleo.
“Nitashirikiana na wenzangu kuifanyia Simba kila linalowezekana ambalo litaonekana ni kubwa. Safari ya hapa Oman nataka pia iwe ni yenye manufaa. Ndiyo maana niliwaambia wachezaji lazima wajitume na kuonyesha muda wao walioutumia hapa ulikuwa na manufaa.
Safari Oman:
Ilikuwa Simba wapelekwe sehemu moja inaitwa Nizwa, ni kama kilomita 150 kutoka hapa Muscat, nikaona si sahihi. Natumia kama milioni 80 au zaidi kuihudumia Simba hapa maana wenyeji wao Fanja nao kama hawaihudumii vilivyo.
Sipendi wafike hapa halafu wateseke, ndiyo maana mambo yote ninayafanya kupitia RBP Group. Najua Simba inajiandaa na nina mpango wa kufanya mengi makubwa ikiwezekana.
Bima:
Tayari tupo katika hatua za mwisho, ndani ya siku moja wachezaji wa Simba na viongozi watakatiwa bima ya maisha. Naamini ni kitu kizuri wakiwa na bima hasa hapa ugenini.
Najua fedha nyingi pia zitatumika lakini naona ni jambo la busara kufanya hivyo, maana sisi ni binadamu na hauwezi kujua kitakachotokea kesho.
Familia, kazi, Simba:
Kweli ni kitu kigumu sana, lakini hayo tayari ni majukumu yangu. Ninapenda kufanya kazi kwa kujituma sana. Wakati mwingine nakesha nikifanya kazi hadi asubuhi maana nina ofisi nyingine Marekani, hivyo kuna vitu navifanya nikiwa hapa Oman au Tanzania, unajua tena dunia sasa ni kama kijiji.
Ugumu utakuwepo lakini sipendi kufeli katika lolote, ndiyo maana napenda kujituma ili nifanikishe kitu ambacho nimekianzisha au nimeingia na kuanza kukifanya.
Ubora:
Ninaamini Simba ni timu bora, lakini lazima wajiandae vizuri na kufanya mambo kitaalamu. Kama watajaribu kubahatisha wataharibu kila kitu. Lakini kujituma pia ni msingi wa maendeleo, hivyo lazima kuwe na watu wenye nia ya kupata mafanikio.
Sisemi Simba itashinda kila siku, lakini ikipoteza basi lazima kuwe na hali ya kukubali, pia ni lazima watu wajitathmini kwa nini wamejikwaa. Mimi pia ninapenda kuona timu yangu inashinda kama ilivyo kwa mashabiki.
Malkia wa Nyuki:
Hili jina nimebatizwa na watu kutokana na tabia yangu ya kupenda kufanya kazi kwa ushirikiano, lakini mara nyingi nimekuwa nikizungukwa na watu ambao wanapenda kuniona nipo salama.
Lakini kifamilia kuna jambo moja, karibu nyumba zangu zote, nyuki wamekuwa wakitengeneza mzinga. Hali hii imewashangaza ndugu na marafiki zangu wengi, hata mimi mwenyewe. Tayari nimelizoea hilo jina na ninaona kawaida ingawa sikulikusudia.
Rahma anaishi katika eneo la Al Kheri, moja ya vitongoji maarufu vya Jiji la Muscat, watu wengi wenye uwezo wa fedha wanaishi eneo hilo.
Nyumba yake inaweza kufikia thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.8, imejengwa kisasa huku ikiwa na mambo kadhaa ya kuvutia utafikiri zile nyumba za mastaa wa Hollywood au wanamuziki maarufu wa Marekani.
Ingawa kuna nyumba nyingi bora katika eneo hilo, bado yake inachomoza pekee na kuonekana moja ya nyumba bora kabisa.
Ukiingia getini, gari inapanda hadi juu ghorofa ya kwanza ambako ndiko kuna sebule, kila moja ikiwa imetengenezwa kwa mfumo wake. Ndani kuna sebule tatu huku kukiwa na vyumba zaidi ya vitano vya kulala.
Kuna vyumba viwili tofauti vya kulia chakula, kuna bwawa la kuogelea lililo ndani ambamo hakuna jua na AC zinawashwa ili kuleta kipupwe. Juu ya bwawa hilo kuna maporomoko ya maji ambayo yanaongozwa na umeme na kuna ukuta wa mawe ambao unafanya eneo hilo liwe kama ziwani.
Mbele ya bwawa hilo la kuogelea kuna ukumbi mdogo ambao bendi au kikundi cha taarabu cha watu kinaweza kutumbuiza na watazamani hadi 70 wakaingia na kuburudika kwa raha zao.
Ndani ya nyumba hiyo kuna ofisi kubwa ikiwa na chumba kidogo cha mikutano ambayo mara nyingi huitumia kufanya kazi zake kama anaamua kutotoka nje.
Kwa kuwa nyumba hiyo inajitosheleza kwa kila kitu, wakati mwingine Malkia huyo wa Nyuki, mama wa watoto pacha, hujikuta akiishi ndani ya nyumba hiyo hata mwezi mzima bila kutoka nje.

SHAFFIH DAUDA MATATANI NA TFF, APEWA SIKU SABA TU ATOE MAJIBU

 
Shaffih Dauda
FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.
 
Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.
 
Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba

Kwa kuipitia barua hiyo bofya: HAPA

HIGUAIN KUFANYIWA VIPIMO LEO NA KUSAINI MKATABA WA MIAKA 3 NA ARSENAL




ARSENAL jana usiku walivunja rekodi yao ya usajili baada ya kukubaliana na Madrid kulipa kiasi cha  £23million kwa ajili ya kumsaini Gonzalo Higuain.

Muargentina huyo atafanyiwa vipimo na Gunners leo na anategemewa kusaini mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya100,000 kwa wiki.

Higuain, 25, amepewa ruhusa na Madrid kusafiri kwenda London baada ya mazungumzo marefu yaliyodumu kwa wiki kadhaa.

Dili hili ambalo limethibitishwa na baba yake Higuain linakuja kuleta nafuu kwa mashabiki wa Arsenal waliokuwa wakililia kocha wao asajili wachezaji wa daraja la dunia, ili kuweza kukata kiu ya zaidi ya miaka nane ya kutwaa kombe.

Santiago Cazorla ndio alikuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Arsenal - akiwa amesajiliwa kwa zaidi ya paundi millioni 16 akitokea Malaga.

Golikipa Julio Ceasar ndio anatajwa kumfuatia Higuain kwenda Emirates akitokea QPR ambao wameshuka daraja.

PICHA ZA WABUNGE WA YANGA WALIVYOWAFUNGA TIMU YA WABUNGE WA SIMBA KWA PENATI 4-3 NA BONGO FLEVA WAIKUNG'UTA TENA BONGO MOVIE KWENYE TAMASHA LA MATUMAINI


Mgeni wa rasmi wa tamasha la matumaini Raisi Jakaya Kikwete akiongozana na marefa kuingia uwanjani tayari kukagua timu za wabunge wa Simba na Yanga

Wimbo wa taifa

JK akisalimiana na timu ya wabunge wa Simba

Mgeni rasmi akisalimiana na upande wa wabunge wa Yanga 
Wabunge wa timu ya Yanga wwakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe kwa kuifunga timu ya wabunge wa Simba kwa penati 4-3.
Bongo Movie kushoto na Bongo Flava kulia wakiiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mechi

Godi Muhokozi wa timu ya Bongo flava akishangilia goli alilolifunga katika kipindi cha kwanza. Pembeni yake ni msanii Abdul Kiba

Msanii wa Wanaume Halisi KR-Mula akishangilia na washabiki wa Bongo Flava..timu hiyo ilishinda 2-0 dhidi ya Bongo movie katika mikwaju ya penati.  


Mbunge wa Sengerema Mh. William Ngeleja akimkabidhi kombe la ushindi nahodha wa timu ya Bongo Flava msanii H-Baba.

TAIFA STARS VS UGANDA JUMAMOSI HII - HIVI NDIO VIINGILIO NA SEHEMU TIKETI ZITAKAPOUZWA


Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayochezwa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani.
Viti vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 kiingilio ni sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 ni sh. 10,000.
Viingilio vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Afrika itachezeshwa na mwamuzi Thierry Nkurunziza kutoka Burundi. Mechi ya marudiano itachezwa jijini Kampala kati ya Julai 26 na 28 mwaka huu.
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo (Ijumaa) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Barbershop iliyoko Sinza Madukani.
Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi.
Tunapenda kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi hiyo

LUIS SUAREZ: "HII NDIO SABABU KWANINI NATAKA KUONDOKA LIVERPOOL"




LUIS SUAREZ hatimaye amekiri sababu rasmi ya kwanini anataka kuondoka Liverpool - anataka kucheza kwenye Champions League.

Mshambuliaji huyo huko nyuma alikaririwa kwenye mahojiano huko Uruguay akisema anataka kuondoka kwa sababu anaandikwa vibaya sana na vyombo vya habari vya kiingereza na kuonewa chama cha soka cha nchi hiyo kwa matendo yake ya kumtukana kibaguzi mchezaji wa Manchester United Patrice Evra na kumng'ata mchezaji wa Chelsea Branislav Ivanovic.

Lakini wakala wake ambaye ni kaka wa kocha wa Bayern Munich, Pere Guardiola amekutana na kocha wa Liverpool Brendan Rodgers mkurugenzi mkuu wa Liverpool Ian Ayre katika uwanja mazoezi wa Liverpool Melwood jana na kuthibitisha kwamba kukosekana nafasi ya kucheza michuano ya ulaya ndio chanzo kikuu cha mteja wake kutaka kuondoka.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameonyesha ishara ya kuwa tayari kulipa kiasi cha £30million kupata saini ya Suarez lakini Liverpool walikataa ofa hiyo wakitaka dau la zaidi £40m.

Real Madrid pia wanatajwa kuandaa ofa nzuri kwa ajili ya kumsaini mshambuliaji huyo.

GARETH BALE NA VAN PERSIE, LEWANDOSKI, MESSI, RONALDO KUGOMBEA TUZO YA MCHEZAJI BORA BARANI ULAYA


GARETH BALE na Robin Van Persie ndio wachezaji pekee kutoka kwenye ligi kuu ya Engalnd ambao wametajwa katika orodha ya wachezaji wanaogambani kinyang'anyiro cha uchezaji bora wa bara la ulaya.

Mabingwa wa ulaya Bayern Munich wametoa wachezaji wanne kwenye listi hiyo, ambayo pia imewahusisha wachezaji Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Tuzo hiyo itatolewa August 29, na jopo la waandishi wa habari barani ulaya ndio watakaopiga kura.
Messi na Andres Iniesta walishinda tuzo hiyo miaka miwili iliyopita. 

NOMINEES: Gareth Bale, Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic, Robert Lewandowski, Lionel Messi, Thomas Muller, Franck Ribery, Arjen Robben, Bastian Schweinsteiger, Robin Van Persie

NIGERIA WATIA AIBU KWA KUPANGA MATOKEO: VILABU VINNE VYAFUNGIWA KWA KUFUNGA MABAO 146 KATIKA MECHI MBILI - WAWEKA REKODI YA DUNIA


Vilabu vinne ambavyo vilihusika na njama ya kupanga matokeo ya mechi vimepigwa marufuku nchini Nigeria.
Katika mechi moja klabu moja iliilaza nyingine magoli 79-0 na magoli 67-0 katika mechi ya pili.
Jumla ya magoli 146 yalifungwa katika mechi hizo mbili, idadi ambayo inaingia katika vitabu vya kumbukumbu kama mechi iliyokuwa na idadi kubwa zaidi ya magoli duniani.
Klabu ya Plateau United Feeders iliilaza timu ya Akurba kwa mabao 79-0 wakati timu ya Polisi ya Machine FC kwa upande wake ikailaza Bubayaro magoli 67-0.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, Muke Umeh amesema ufisadi na ulaghahi wa kiwango hicho hakiwezi kukubalika katika soka ya sasa.
Umeh ametangaza kuwa baada ya mkutano wa kamati hiyo, ilibainika wazi kuwa vilabu hivyo vina kesi ya kujibu na hivyo vyote vinne vimepigwa marafuku ya kushiriki katika mecho yoyote, hadi uchunguzi utakapokamilika.
Kabla ya mechi hiyo vilabu vya Plateau United Feeders na Police Machine vilikuwa na alama sawa na vilikuwa vikipania kupandishwa daraja hadi ligi daraja ya pili.
Feeders ilipata magoli 72, katika kipindi cha pili ili hali Machine nao wameripotiwa kufunga magoli 61 katika kipindi cha mechi yao.
Kufuatia matokeo hayo Plateau ilimaliza ya kwanza kwenye msimamo wa ligi na idadi kubwa ya magoli ikifuatwa na timu hiyo ya polisi.
''Tutachunguza sakata hii na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika'' Alisema Ummeh.
Mkurugenzi wa michezo na mashindano wa Shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, Dkt. Mohamed Sanusi, amekariri tangazo lililotolewa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi kuwa waliohusika wataadhibiwa vikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NFF, vilabu vilivyohusika, wachezaji,, maafisa wa kiufundi wa timu na wasimamizi wa mechi hiyo watakaopatikana kuhusika kwa njia moja au nyingine, katika kashfa hiyo ambayo imetajwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya soka nchini Nigeria watachukulia hatua kali za kisheria.

WAAMUZI WALIOPANGWA KUCHEZESHA MECHI YA STARS VS UGANDA WAFELI MTIHANI WA WAAMUZI - WABADILISHWA



Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefanya mabadiliko ya mwamuzi wa mechi ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi aliyeondolewa kutokana na sababu za kiufundi ni Jean Claude Birumushahu aliyekuwa mwamuzi msaidizi namba moja. Nafasi yake sasa inachukuliwa na Herve Kakunze pia kutoka Burundi.
CAF imemuondoa mwamuzi huyo baada ya kufeli katika mtihani wa waamuzi (Cooper Test) kwa waamuzi wa Burundi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) uliofanyika nchini humo siku tatu zilizopita.
Waamuzi hao na Kamishna wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea wanatarajiwa kuwasili nchini kesho (Julai 11 mwaka huu) kwa ndege za Kenya Airways na EgyptAir kwa muda tofauti.
Nayo Uganda Cranes inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Julai 11 mwaka huu) na itafikia hoteli ya Sapphire. Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) bado halijatuma taarifa rasmi juu ya ujio wa timu hiyo.
Wakati huo huo, makocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen na wa Uganda, Milutin Micho pamoja na manahodha wao watakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika keshokutwa (Julai 12 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF kuzungumzia mechi ya Jumamosi.

QATAR KUTUMIA $200 BILLIONI KWA MAANDALIZI YA KOMBE DUNIA 2022 - KUJENGA VIWANJA KAMA CHA BARCA NA VYENYE AIR CONDITION



Kujenga viwanja vyenye air-condition na vyenye uwazi kwa juu katika jangwa ni gharama sana. 
Kampuni ya Deloitte imesema kwamba Qatar itatumia $200 billion katika kipindi cha miaka 10 ijayo wakati ikijiandaa kuandaa 2022 World Cup, the Associated Press imeripoti.
Fedha hizo zitatumika kwenye miundombinu ya usafiri na utalii pamoja na viwanja vipya. Zaidi ya mashabiki 400,000 wanategemewa kwenda kwenye nchi hiyo kwa ajili ya michuano hiyo itakayochukua mwezi mmoja kufanyika.
Wakati michuano hiyo ikipangwa kufanyika kwenye wakati wa kiangazi, joto hupanda kwa kiasi kikubwa sana, Qatar inajipanga kujenga viwanja vyenye air-condition, pamoja na vyenye uwazi kwa juu ambavyo vyote vitakuwa vikitumia umeme wa nguvu za jua.

UGANDA CRANES YAWASILI KUIKABILI STARS


Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) imewasili Dar es Salaam leo tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) kati yake na Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
The Cranes inayofundishwa na Mserbia Sredojvic Micho imetua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda, na imefikia hoteli ya Sapphire.
Timu hiyo leo (Julai 11 mwaka huu) itafanya mazoezi saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Karume, wakati kesho saa 9 alasiri itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, kabla ya kuipisha Taifa Stars itakayoanza mazoezi saa 10 kamili jioni.
Taifa Stars inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen, na kudhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, leo kwa mujibu wa program yake haitakuwa na mazoezi.
Wachezaji wanaounda The Cranes ni makipa Ismail Watenga, Kimera Ali na Muwonge Hamza. Mabeki ni Guma Dennis, Kasaaga Richard, Kawooya Fahad, Kisalita Ayub, Magombe Hakim, Malinga Richard, Mukisa Yusuf, Savio Kabugo na Wadada Nicholas.
Viungo ni Ali Feni, Birungi Michael, Frank Kalanda, Hassan Wasswa, Kyeyune Said, Majwega Brian, Mpande Joseph, Muganga Ronald, Ntege Ivan, Owen Kasule, wakati washambuliaji ni Edema Patrick, Herman Wasswa na Tonny Odur.

KURUDI KWA LUKAKU - JE CHELSEA INAMUHITAJI BENTEKE? KUONDOA UTEGEMEZI KWA BALE - SPURS LAZIMA ISAMJILI BENTEKE


Baada ya kuwa na msimu mzuri wa kwanza katika  Premier League, hatma ya Christian Benteke ndani ya Aston Villa haieleweki baada ya kuomba kuuzwa rasmi huku akiwa na matumaini ya kwenda klabu kubwa zaidi. Sio kusema kwamba Aston Villa sio klabu kubwa lakini ukubwa unaotazamwa siku hizi ni ule wa pochi la kulipa mishahara mikubwa na kusajili mastaa wenye majina makubwa. Lakini je Benteke ni mchezaji wa daraja la kiasi hicho?
Akisajiliwa kwa kiasi cha £7m wakati wa dirisha kubwa la usajili msimu uliopita, wengi walidhani Aston Villa wamelipa fedha nyingi  kwa mshambuliaji huyo wa Kibelgiji, lakini Banteke amethibitisha thamani yake baada ya kufunga mabao 19 katika premier league - 14 kati ya hayo ameyafunga ndani ya miezi 5 ya mwaka 2013, mengi kuliko mchezaji yoyte wa premier league.
Aston Villa tayari wameshesema kwamba Benteke ataondoka kwenye klabu hiyo ikiwa tu watapata fedha inayostahili, ambayo inatajwa kuwa ni zaidi ya £20m. Umuhimu wa Benteke kwa Villa sio kitu cha kushangaza kwa kuwa mchezaji huyo alifunga asilimia 40 ya mabao yote ya Villa msimu uliopita na kuwasaidia wasishuke daraja. 
Timu zinazoripotiwa kuvutiwa na kumsajili Benteke ni Chelsea na Tottenham, ambao wote wanataka kuboresha safu zao za ushambuliaji kabla ya msimu mpya.
Hatma ya Torres na Demba Ba ndani ya Chelsea haijaeleweka huku tetesi zikisema wanaweza wakaondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuhangaika kucheza kwenye kiwango kwa muda mrefu, lakini huku Lukaku akirejea darajani akitokea West Brom alipokuwa kwa mkopo - ni kweli Benteke anahitajika ndani ya Stamford Bridge?
Wabelgiji hawa wawili kila siku wamekuwa wakifananishwa wakiwa wanagombea nafasi ya kucheza kama mashambuliaji kwenye timu y taifa, lakini ni vigumu sana kuamua yupi bora zaidi ya mwenzake.
Ukijaji kwa kupitia msimu uliopita, Benteke alimfunika Lukaku kwenye ligi kwa mabao 19 dhidi ya 17 na alikuwa mshambuliaji namba moja kwenye timu ya taifa wakati wote wa michuano ya kugombea kufuzu kucheza kombe la dunia. Lukaku ingawa alianza michezo kadhaa.

TAKWIMU ZINASEMAJE KUHUSU WACHEZAJI HAWA WAWILI
Benteke Lukaku Benteke   Ready for a step up? Stats compared to Lukaku & Adebayor
Lukaku aliweza kufunga goli kila baada ya dakika 118 ukilinganisha na Benteke ambaye aliweza kufunga goli kila baada ya dakika 149. Lukaku pia aliweza kupiga mashuti mengi golini - yaliyolenga lango na yaliyotoka nje (47 and 34), huku mashuti yaliyolenga lango akipiga moja kila baada ya dakika 43 wakati mashabiki wa Villa iliwalazimu kusubiri dakika 66 kuona shuti la Benteke likilenga lango - nii kwa kiasi inaonyesha namna watu hawa wawili wanavyotofautiana.
Lukaku anaweza kwenda pembeni wakati wa mashambulizi jambo ambalo litaipa uhuru nafasi ya kiungo - labda kumpa uhuru mtu kama Lampard kuingia ndani ya box - na hili linaweza kuonekana wakati akiwa na West Brom ambapo aliweza kupiga krosi 58. Benteke pia anaweza kufanya hivi, lakini siokwa kiasi kikubwa kama Lukaku - msimu uliopita aliweza kupiga krosi 11 tu kuingia ndani ya box.
Tottenham wanakuja kuanza kumtaka Benteke baada ya kumkosa mshambuliaji  David Villa wakiwa wanamtafuta mfungaji halisi na sio kumtegemea Gareth Bale peke yake - wakiwa na washambuliaji wawili tu halisi ndani ya kikosi.
 
Jermaine Defoe alianza vizuri msimu uliopita lakini alifunga bao 1 tu ndani ya miezi 5 ya mwaka 2013, wakati Adebayor ni kivuli cha mchezaji aliyekuwa Spurs kwa mkopo kabla ya kusajiliwa moja kwa moja. Mtogo huyo alifunga mabao 17 na kutoa assists 11 katika msimu wa 2011/12, wakati kwenye msimu uliopita alifunga mabao 5 na kutoa assist 1.
Adebayor Benteke   Ready for a step up? Stats compared to Lukaku & Adebayor

Kukosekana kwa mabao kutoka kwa washambuliaji msimu uliopita kulipelekea Tottenham kukosa nafasi kwenye Champions League, kitu ambacho Benteke angeweza kuwasaidia. Mchezaji huyo wa Villa alikuwa na wastani wa  26% kutumia nafasi za kufunga nyingi kuliko Adebayor aliyekuwa na wastani wa asilimia 17.
Wakati Christian Benteke akiwa amewavutia watu wengi kwenye Premier League mpaka sasa, mashaka juu yake yataendelea kuwepo mpaka pale atakapoendeleza mauaji yake ndani ya msimu ujao na kuthibitisha hakubahatisha msimu uliopita. 
Huku Lukaku akirejea na wakiwa fedha za kutumia, Chelsea wataongeza mshambuliaji mwingine kwenye kipindi hiki cha kiangazi. Tottenham nao wanaweza wakawa chaguo sahihi kabisa kwa Benteke ambaye atakuwa akicheza katikati ya mawinga Bale na Lennon ambao kwa hakika watamsaidia sana kung'ara kuliko alivyokuwa Villa lakini hilo litatokea ikiwa tu watalipa fedha ambayo Villa wanaitaka.