LUIS SUAREZ hatimaye amekiri sababu rasmi ya kwanini anataka kuondoka Liverpool - anataka kucheza kwenye Champions League.
Mshambuliaji huyo huko nyuma alikaririwa kwenye mahojiano huko Uruguay akisema anataka kuondoka kwa sababu anaandikwa vibaya sana na vyombo vya habari vya kiingereza na kuonewa chama cha soka cha nchi hiyo kwa matendo yake ya kumtukana kibaguzi mchezaji wa Manchester United Patrice Evra na kumng'ata mchezaji wa Chelsea Branislav Ivanovic.
Lakini wakala wake ambaye ni kaka wa kocha wa Bayern Munich, Pere Guardiola amekutana na kocha wa Liverpool Brendan Rodgers mkurugenzi mkuu wa Liverpool Ian Ayre katika uwanja mazoezi wa Liverpool Melwood jana na kuthibitisha kwamba kukosekana nafasi ya kucheza michuano ya ulaya ndio chanzo kikuu cha mteja wake kutaka kuondoka.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameonyesha ishara ya kuwa tayari kulipa kiasi cha £30million kupata saini ya Suarez lakini Liverpool walikataa ofa hiyo wakitaka dau la zaidi £40m.
Real Madrid pia wanatajwa kuandaa ofa nzuri kwa ajili ya kumsaini mshambuliaji huyo.
No comments:
Post a Comment