Pages

Saturday, July 13, 2013

JUNINHO KUCHEZA BURE VASCO DA GAMA ILI ALIPWE MADENI YAKE YA NYUMA


Mchezaji wa zamani wa Brazil Juninho Pernambucano anatarajia kucheza bure baada ya kurudi kwenye timu ya Vasco de Gama.

Kiungo huyo mwenye miaka 38, ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo katika vipindi viwili tofauti, anajiandaa kurudi kwa kipindi cha tatu kwenye klabu hiyo yenye maskani yake ya Rio De Jeneiro ambapo hatopata mshahara.

Badala yake, nyota huyo wa zamani wa Lyon ameripotiwa atapokea malipo ya madeni yake yote ya zamani anayoidai klabu hiyo.  

Inaeleweka kwamba Juninho atarudi kujiunga na klabu hiyo ya Brazil kwa miezi sita kabla ya kutundika daluga zake. 

Mapema mwezi huu alimaliza mkataba wake na klabu ya MLS  New York Red Bulls baada ya miezi saba, ambapo alikatisha mkataba wake akitoa sababu binafsi ndio zilizosababisha

DROGBA KUJENGA HOSPTALI TANO NDANI YA IVORY COAST KWA AJILI YA WATOTO NA WANAWAKE


Kupitia taasisi yake ya kutoa misaada, nahodha wa Ivory Coast na gwiji wa Chelsea Didier Drogba atasaidia ujenzi wa kliniki tano za watoto na wanawake katika nchi yake. Tangazo hilo lilitolewa na katibu mkuu wa Didier Drogba Foundation Guy Roland Tanoh, ambaye alisema kwamba ujenzi wa kliniki hizo utafadhiliwa na Taasisi ya London galas pamoja na fedha Drogba mwenyewe.
Kutoka SuperSport:
Tanoh amesema kiasi cha 2.5 billion CFA francs ($5 million) kitatumika kuwekeza katika ujenzi wa kliniki hizo, huku zikijengwa katika miji mitano mikubwa ya nchi hiyo Abidjan, Yamoussoukro, Man, Korhogo na San Pedro.
“Drogba aliendesha mchango huko London na zikapatikana kiasi cha $ 2 billion CFA francs ($4 million),” Tanoh alisema. “Kiasi kilichobakia cha million francs ($1 million) hakitakuwa tatizo kuona ndoto ya mwenyewe Drogba ya kuona afya za wananchi wa Ivory Coast zinapewa kipaumbele.”
Drogba mara ya kwanza alitangaza mpango wake wa kujenga hospitali kubwa katika jiji la Abidjan mwaka 2009 akitumia fedha zote - kiasi cha £3 million ($4.5 million) alicholipwa na Pepsi. Lakini badala ya kujenga hosptali hiyo moja kubwa akaamua ambayo ingekuwa mjini tu, akaamua kujenga vituo vitano vya afya katika mikoa mingine ili kuweza kusambaza vizuri huduma za afya.

MESSI: NINA DENI KWA RONALDINHO



Lionel Messi amefunguka na kusema ana deni kubwa la shukrani kwa Ronaldinho kwa namna alivyoweza kumsaidia wakati anaingia kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona.

Mshindi huyo wa mara wa tuzo ya Ballon d'Or aliingia kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza cha Barca mwaka 2004, mwaka mmoja baada ya Dinho kuwasili Nou Camp akitokea Paris Saint-Germain.

Huu ni wakati Messi anasema hatokuja kuusahau kwenye maisha na anakiri ukarimu wa Ronaldinho pamoja na kuwa staa mkubwa kumliko ulimfanya azoee kwa haraka maisha ya kikosi cha wakubwa cha Barca. 

"Siku zote nimekuwa nikisema, siku tu nilipoingia chumba cha kubadilishia nguo Ronaldinho na wenzie Deco, Sylvinho na [Thiago] Motta walikaniribisha na kunipa baadhi ya vifaa, lakini zaidi ni Ronaldinho ambaye pia alinifundisha vitu vingi uwanjani na nje ya dimba," Messi aliiambia Barca TV"Ulikuwa ni msaada mkubwa. Ni vigumu kuenda kwenye timu ya mastaa kama Ronaldinho na kupata ukarimu kama wake. Alifanya kila kitu kikawa rahisi kwangu. Nilikuwa na bahati kuwa karibu nae na kushea vitu vingi.

"Ninaweza kusema Ron ni mtu mzuri sana na hicho ndio kitu muhimu."
Ronaldinho aliiwezesha Barca kubeba makombe mawili ya Liga na Champions League wakati wa miaka yake mitano aliyoitumikia klabu hiyo ya Camp Nou na Messi anaamini kiungo huyo mwenye miaka 33 ana mchango mkubwa kwa mafanikio aliyonayo sasa.

"Ronaldinho ndio mtu aliyeleta mabadiliko makubwa kwenye klabu hii," anasema. "Klabu ilikuwa inapitia wakati mmoja m'baya sana lakini hali hiyo ilibadilika mara tu alipowasili. Msimu wake wa kwanza hatukushinda chochote lakini watu walimpenda sana. Baadae yakaja mataji na akawapa furaha watu wengi sana

JE TAIFA STARS ITAWEZA KUFUTA UTEJA NA KULIPA KISASI KWA UGANDA KWENYE MICHUANO YA CHAN???



Leo Jumamosi tarehe 13, July: Tanzania itapambana na Uganda kwenye uwanja wa taifa katika mchezo wa kugombea nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza kwenye ligi za ndani. 

TAARIFA ZA TIMU YA UGANDA:

Uganda Cranes ilitua Bongo wakitokea kwao siku ya alhamisi. Kikosi cha wachezaji 18 na kufikia kwenye hotel ya Sapphire iliyopo katikati ya jiji la Dar es salaam wakionekana kuwa kwenye hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa leo katika dimba la uwanja wa taifa unaoweza kubeba mashabiki zaidi ya 55,000. 
Uganda wanatarajiwa kuchezesha wachezaji wengi wapya kwenye hatua hii ya kimataifa. Ukimuacha mlinzi Dennis Iguma na kiungo Wasswa Mawanda, ambao walicheza dakika zote 90 kwenye mchezo wa kugombea kwenda Brazil 2014 dhidi ya Liberia na Angola, wachezaji wote waliobakia bado hawajaonja utamu wa soka la kimatiafa. 
Hakuna beki wa kushoto asilia kwenye kikosi hiki cha Micho, ukizingatia mchezaji aliyeitwa kuja kucheza kwenye nafasi hiyo  Habib Kavuma, aliondolewa kikosini baada ya kugundulika kwamba alipewa kadi nyekundu kwenye mchezo wa 2011 CHAN dhidi ya Gabon. Hili linamuacha Micho Akibakiwa na mbadala Yusuf Mukisa, beki wa kulia ambaye hujaribu kucheza nafasi hiyo pia.
Wachezaji wengine ambao wana uzoefu kidogo na michuano ya CHAN ni Ayubu Kisaliita, Patrick Edema, Tonny Odur Hamuza Muwonge, ambao walicheza kwenye michuano ya CHAN iliyofanyika Khartoum, Sudan.
Kutokana kuwa ugenini - Micho anategemewa kuipanga timu yake huku akicheza mchezo wa kuzuia sana na kushambulia kwa kushtukiza. Uganda wanaweza kuanza kwa mfumo wa 4-2-1-3, baadae wakibadilika kuja 4-3-3 na 4-4-2 kadri muda unavyozidi kusogea.


MCHEZAJI WA KUCHUNGWA: Dennis Iguma


Dennis Iguma ameimarika sana kwenye kiwango chake, kujiamini kwake na namna anavyojua kucheza kitimu. Mchezaji huyu ambaye alitumia utoto wake kupata mafundisho ya soka kupita chuo cha soka cha Entebbe, anaweza kucheza popote uwanjani kwa kiwango kile kile anachocheza kwenye nafasi yake ya kawaida. 
Iguma, kwa sasa anaichezea klabu ya Sports Club Victoria University anategemewa kuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Stars wakiongozwa na Canavaro na Yondani.
TANZANIA:
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemrudisha kikosini beki wa kulia wa Yanga, David Luhende akitoa picha kwamba Shomary Kapombe beki halisi wa kulia atahamia upande wa kushoto. Hii inakuja baada kumpa mapumziko Nyoni ambaye alicheza ovyo kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Morocco na Ivory Coast.
Huku Uganda ikiwa ndio timu iliyo juu kisoka kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, kocha wa Tanzania alizungumza na kusema yafuatayo."Utakuwa mchezo mgumu sana kwetu kwa sababu Uganda ni timu nzuri; tumekuwa hatuchezi vizuri sana dhidi yao katika mechi za hivi karibuni." 
Wakiwaondoa washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu, ambao wanacheza TP Mazembe ya DR Congo, Taifa Stars itakuwa na wachezaji saba ambao walicheza kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia 2014. 
MCHEZAJI WA KUCHUNGWA: Amri Kiemba
Kiungo huyo wa kimataifa wa Simba amekuwa na kiwango kizuri sana kuanzia msimu uliopita kwa Timu yake ya klabu na sasa kwenye timu ya taifa. Ana akili ya mpira, anatuliza mashambulizi na kupeleka mashambulizi kwa adui pamoja kuwatengenezea nafasi wenzie. Ikiwa atacheza kwenye kiwango chake cha juu basi Uganda watapata taabu sana kumchunga Kiemba asiweze kuwadhuru.

TIMU ZINAZOWEZA KUANZA



CRANES  XI (4-2-1-3):
                            Hamuza Muwonge (GK)
Nicolas Wadada - Savio Kabugo - Richard Kasagga - Yusuf Mukisa
                           Hassan Wasswa (Captain) -Dennis Iguma
                                    Joseph Mpande
               Tonny Odur -Patrick Edema - Ronald Muganga
TANZANIA XI (4-3-3)
                             Juma Kaseja (GK)- Captain
Shomari Kapombe - Yondan - Nadir 'Canavaro' Haroub - David Luhende
                           Sure Boy - Frank Domayo
                                   Mwinyi Kazimoto
               Mrisho Ngassa-John Bocco - Amri Kiemba
JE WAJUA ?
- Mpaka kufikia 12th July 2013, Uganda inashika nafasi ya 80 katika listi ya timu bora duniani ya FIFA - wakati Tanzania ikishika nafasi ya 121 na pointi 271.
Uganda Cranes ilifuzu kucheza 2011 CHAN Championships jijini Khartoum, Sudan kufuatia kuifunga Tanzania nyumbani na ugenini.
- Uganda ilifunga goli moja katika CHAN iliyopita iliyofanyika Sudan. Ibrahim Saddam Juma alifunga goli dakika ya 77 dhidi ya Gabon.

- Kocha wa Uganda, atakuwa anaiongoza UG kwa mara ya nne tangu amrithi Bobby,  ameshacheza dhidi ya Libya katika mechi ya kirafiki na kufungwa 3-0, akaja kushinda 1-0 na 2-1 dhidi ya Liberia na Angola katika mechi za kufuzu kombe la dunia 2014.



Tanzania iliwahi kushirikia michuano hii wakati tu ilipoanzishwa na kufanyika nchini Ivory Coast

SIMBA YAIPIGA BAO YANGA - YAMSAJILI HAMIS TAMBWE KWA MIAKA 2


Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imefanikiwa kumsajili mfungaji bora wa michuano ya Kagame Cup 2013 Hamis Tambwe kutokea Vital O ya Burundi.

Tambwe ambaye pia alikuwa akiwania na mabingwa wa Tanzania bara Yanga, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba.
Tambwe amesaini mkataba huo mbele ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba.

KWA MARA YA KWANZA TANZANIA;BAADA YA KUSHUKA DARAJA - AFRICAN LYON YATANGAZA KUPATA HASARA YA MILLIONI 180.3


TIMU ya soka ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam imetangaza hasara ya sh. milioni 180.3 kutokana na ushiriki wake katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lyon ni miongoni mwa timu tatu zilizoshuka daraja kutoka katuika ligi hiyo kubwa ya soka nchini, nyingine ni Toto African na Polisi Moro.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Meneja wa Fedha wa Lyon, Ibrahim Salim, alisema timu yao imetumia zaidi ya sh. 388,614,500 kwa ajili ya maandalizi hadi michezo yake.


Salim alisema katika makusanya na matumizi yao, walilazimika kutumia kiasi cha sh. milioni 268.09 katika mzunguko wa kwanza, kabla ya kutumia sh. 123.6.

"Katika matumizi yote haya, fedha ambayo tumeiingiza kama klabu kupitia viingilio na vyanzo vingine ni sh. milioni 207.6, na hapo ndipo unapopata tofauti ya sh. milioni 180.3, ambayo ni hasara," alisema Salim.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Lyon, Rahim Kangezi, alisema soka ya Tanzania inaendeshwa kwa hasara huku wenye dhamana ya kusaidia wakiwa hawatendi haki kwa baadhi ya vipengele.

Kangezi alisema timu yake imeingia katika hasara ya sh. milioni 180.3 kutokana na uendeshaji, lakini bado wameshuka daraja, huku akisisitiza kuwa hakuna anayeshutumiwa kwa kushuka kwa timu hiyo.

"Unaweza kuona changamoto ambayo tunakumbana nayo katika uendeshaji wa taasisi kamam a hizi, tunapopiga kelele kwa wadhamini kutuwahishia fedha tunamaanisha.

"Angalieni mfano mdogo kwa fedha za wadhamini (Vodacom), ambazo awamu ya mwisho zimetufikia Mei mwaka huu, tukiwa tumebakiza mechi moja ya Ligi Kuu, sasa zingetusaidia katika nini? Alihoji mmiliki huyo.

Akizungumzia kuhusu uendeshwaji wa Ligi Kuu na changamoto walizokutana nazo, Kangezi alisema bado hakujakuwa na usimamizi mzuri katika kuhakikisha kuwa ligi hiyo inakuwa bora.

Katika hatua nyingine, Kangezi alisema timu yake inajivunia mafanikio waliyochangia kusogeza maendeleo ya soka nchini kutokana na kutoa nafasi kwa Mrisho Ngassa kwenda kujaribu soka ya kulipwa na kucheza katika kikosi cha Seattke Soundowns dhidi ya Manchester United.

"Tulifanikiwa pia kuileta timu kubwa ya Ligi Kuu ya Brazil (Atletico Parenese) kwa ziara ya kimichezo nchini, tulitoa wachezaji watano kwa ajili ya kujaribu soka ya kulipwa sambamba na kufanya semina mbili juu ya uongozi wa michezo," aliongeza

REAL MADRID WAMSAJILI RASMI MRITHI WA XABI ALONSO KWA ADA YA UHAMISHO WA £33.6m


Real Madrid wamekamilisha usajili wa kiungo wa Real Sociedad Asier Illarramendi kwa ada ya uhamisho wa £33.6m - Illarramendi ni kiungo wa timu ya taifa ya Spain chini ya umri wa miaka 21 na anatajwa kuwa ndio mrithi wa  Xabi Alonso.

Mhispania huyo amehamia Bernabeu kufuatia kucheza kwa kiwango kikubwa sana kwenye michuano ya Euro Under 21 mwezi uliopita.Real Madrid tayari imeshamsajili Daniel Carvajal, Isco na Casemiro kabla ya ujio wa kocha Carlo Ancelotti kutoka PSG, hivyo usajili wa Illarramendi unakuwa wa kwanza kufanyika chini ya kocha huyo muitaliano.

Illarramendi ana sifa za uchezaji kama ilivyo kwa kwa kiungo wa zamani wa Liverpool Xabi Alonso na anatajwa kuwa ndio mtu anayeandaliwa kumrithi Alonso kwenye timu ya taifa na sasa Real Madrid

MPIRA WA RONALDO,MESSI MIGUUNI MWA NEEYMAR


Neymar 

NEYMAR ameanza ufalme wa dunia, itabaki kuwa hivyo mpaka Lionel Messi na Cristiano Ronaldo watakapochangamsha buti zao kwa mara nyingine.
Mwanasoka huyo amedhihirisha hilo kwenye Kombe la Mabara. Michuano hiyo imempandisha daraja na kuonyesha kwamba yupo sambamba na mastaa hao wawili bora katika Dunia ya soka la kisasa.
Bahati nzuri ni kwamba La Liga, ndiyo itakayowashuhudia wachezaji wote watatu wakicheza msimu ujao, Neymar akiungana na Messi katika kikosi cha Barcelona kuendeleza upinzani dhidi ya Real Madrid inayotawaliwa na Ronaldo.
Kwa kipindi chote za Kombe la Mabara, Neymar alionyesha kile kilichowafanya Barca wamsajili na kile kilichokuwa kikiwasukuma Real Madrid wafukuzie saini yake kwa muda mrefu. Wakati huu, yeye ni namba moja.
Si mchezaji unayeweza kumtumia tu kama mapambo kwenye majarida na shughuli za kibiashara, Neymar ni mchezaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kuamua matokeo ya mechi na anayesaidia kutwaa mataji.
Alicheza michuano yake ya kwanza mikubwa akiwa na kikosi cha Brazil kwa usahihi kabisa. Achana na habari kuwa huenda akachelewa kulifahamu soka la Ulaya, kukosa nguvu au mambo mengine, Neymar ni fumbo zito kwa Messi na Ronaldo, ambalo kwa sasa wanapaswa kulifumbua kama wanahitaji kuendelea kuwa juu.
Mbrazili huyo aliwavaa na kuwachachafya wapinzani wake wa timu zote alizocheza nazo katika mechi tano kwenye michuano ya Kombe la Mabara. Kiwango chake kwenye mechi ya fainali, dhidi ya Hispania kilibainisha uwezo wa Neymar ulivyo.
Pasi aliyopiga kwa Oscar kabla ya kufungua nafasi ambapo kiungo mchezeshaji wa Chelsea alimrudishia tena mpira na kufumua shuti kwa mguu wa kushoto lililomshinda kipa, Iker Casillas, imeonyesha Neymar si mchezaji wa kufikirika bali ni halisi.
Neymar hakutaka kucheza na kamera zilizokuwa zikimmulika kama wengi walivyokuwa wakidhani katika michuano hiyo, alifanya kazi na kufanikiwa kuipa taji muhimu timu yake.
Wakati filimbi ya mwisho ya michuano hiyo inapulizwa kwenye Uwanja wa Maracana, Neymar alinyakua tuzo ya Mchezaji Bora na kuwazima waliokuwa wakibeza kwamba yeye si mchezaji wa mechi kubwa.
Ikumbukwe kuwa Neymar ndio kwanza ana umri wa miaka 21, hilo linawafanya Messi na Ronaldo kukuna vichwa. Ni wazi Ronaldo anapaswa kuweka ‘ubishoo’ kando na Messi afute mawazo ya kwamba kila kitu ni yeye pale Nou Camp.
Neymar aliingia kwenye gumzo la usajili kwa takribani miaka miwili iliyopita, hakika huo ulikuwa uamuzi bora  wa kuamua kubaki Brazil mahali ambapo aliweza kujiweka sawa kabla ya kutua Ulaya akiwa amesogea kwa namna fulani katika kuwanyima raha Ronaldo na Messi.
Uzuri uliopo ni kwamba anakwenda Ulaya katika mwaka wa kuelekea fainali za Kombe la Dunia, jambo ambalo litampa hamasa ya kufanya vyema ili awemo kwenye kikosi cha taifa lake la Brazil. 
Kutoendelea kucheza nyumbani katika ligi ambayo haikuwa na ushindani sana ikilinganisha na ligi za Ulaya, kutamsaidia Neymar kupandisha kiwango chake kiuchezaji.
Sasa kila mmoja anamfahamu Neymar ni nani kwa kuitazama michuano ya Kombe la Mabara, ambapo Hispania kwenye mechi ya fainali walishikwa vilivyo na kinda huyo pamoja na umaarufu wao wa kupiga pasi ndani ya uwanja.
Wakati jina la Neymar likianza kuchomoza, Dunia bado inaimba majina ya akina Messi na Ronaldo, lakini kwa kuwa Neymar tayari ametua kwenye bara la Ulaya, kibao kitaanza kubadilika. Sasa Mbrazili huyo atatawala mazungumzo katika vijiwe vya soka.
Tayari ameshatajwa mara mbili kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Marekani ya Kusini jambo ambalo litamsumbua Messi kwenye Ballon d’Or ambako amekuwa mtawala kwa miaka minne mfululizo.
Kinachosubiriwa kwa sasa ni kuona Neymar anaikamata La Liga na Kombe la Dunia 2014 ili aishike rasmi Dunia. Sawa fedha zimemtoa Brazil na kuhamia Ulaya, lakini  uhamisho wake wa Barcelona unafaida kubwa katika ukuaji wa soka lake na hapo ni mahali pazuri ambapo ataliweka jina lake katika kurasa za kihistoria.
Kwa vyovyote itakavyokuwa kwa sasa, nyota ambaye  anatazamiwa kuwa gumzo katika fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil ni Neymar na si Ronaldo au Messi. Katika klabu ya Barcelona si kwamba yeye aliitaka timu hiyo bali wababe hao wa Catalan ndio waliotaka huduma yake, kutokana na hilo ni lazima watamtafutia nafasi ya kuwamo kwenye kikosi.
Kwa wakati huu, Barcelona inaonekana kuwa ni timu ya Messi kwa sababu ataendelea kuwa mahali hapo, jambo hilo halimfanyi Neymar kuonekana si kitu lakini ni wazi kiwango chake kitaanza kumtia presha Muargentina huyo na umaarufu wake ndani ya Camp Nou.
Akisubiri mwaka mmoja wa taifa lake kuandaa fainali za Kombe la Dunia, Neymar amepata nafasi ya kucheza kwenye klabu bora duniani, tena sambamba na wachezaji wajuzi kama Xavi na Iniesta pamoja na Messi, hilo litamkomaza zaidi katika kufanya mapinduzi ya utawala katika mchezo huo.
Neymar atakuwa na nafasi ya kufahamu soka la kimataifa lipoje, si tu Kombe la Dunia, Copa America, Copa Libertadores na Kombe la Mabara, hapa atapata fursa ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambayo imekuwa ikishirikisha timu bora za klabu na zenye wachezaji kutoka pande tofauti katika Dunia hii.
Kwa siku za karibuni, Neymar ameweza kuonyesha kukomaa na si kama ilivyokuwa awali ambapo alikuwa akigongwa kidogo tu anakwenda chini.
Ukomavu huo wa sasa unaweza kuimarika zaidi wakati atakapojiunga na Barcelona kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
Presha ya kikosi cha Brazil kwenye Kombe la Dunia kwa sasa inamhusu Neymar. Tayari ameanza kukomazwa na kuwekwa kwenye fungu la wachezaji mahiri kama ilivyokuwa kwa Pele, Zico, Ronaldo na Ronaldinho.
Kizazi kipya cha Brazil kina wachezaji kama Dani Alves na Thiago Silva, ambao wana uzoefu mkubwa wa kucheza ligi kubwa barani Ulaya tofauti na Neymar, lakini presha ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia inaendelea kumwandamana kinda huyo.
Kiwango chake cha uchezaji kinapita kwenye hatua nzuri, swali lililopo je, ataweza kuishinda presha ya Kombe la Dunia? Kama atafanikiwa kuishinda vita hiyo, hakika atakuwa amewaweka ‘mfukoni’ Messi na Ronaldo