Pages

Friday, July 12, 2013

JUMA KASEJA KUWA MRITHI WA CASSILAS MTIBWA SUGAR


ENDAPO Mtibwa Sugar ya Morogoro itamuuza kipa wake namba moja, Hussein Shariff ‘Casillas’ kwa FC Lupopo ya Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Congo imepanga kumsajili Juma Kaseja ambaye amemaliza mkataba wake na Simba.
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime alisema Casillas amefuzu Lupopo na kinachofanyika sasa ni makubaliano ya dau.
 “Iwapo tutamuuza Casillas, tutamsajili kipa mwingine bora kama Juma Kaseja ili kuhakikisha tunabaki katika hali nzuri na kumudu vyema mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.”
Mwezi uliopita, Hussein Sharif alinyakua tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka  ya Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza) na kuwafunika makipa wa Taifa Stars, Juma Kaseja na Mwadini Ali. Shariff atakuwa anatoka nje ya nchi kwa mara ya pili kwenda kucheza soka la kulipwa baada ya awali kushiriki Ligi Kuu Msumbiji mwaka 2008.
Wakati huohuo, kocha wa timu hiyo na pia nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Maxime alisema Mtibwa inazingoja klabu za Simba na Yanga kumaliza fujo za usajili na ndipo wao waanze.
Katika hatua nyingine, Coastal Union ya Tanga imekana kufanya mazungumzo ya usajili na Kaseja.
Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo ya Tanga, Nassor Binslum alisema klabu hiyo kuwasajili wachezaji wenye majina kama Haruna Moshi ‘Boban’ na Juma Nyoso haina maana kuwa ndio wamsajili Kaseja.
 “Tunatambua kuwa Kaseja ni kipa mzuri sana, lakini hana nafasi Coastal, usajili wa kina Boban ulifanyika kwa sababu tuliwahitaji kutokana na kupungukiwa na wachezaji na si kwa sababu

No comments:

Post a Comment