USAJILI wa wanasoka barani Ulaya umeanza kupamba moto, tumeanza kuona nyota kadhaa wakinaswa.
Wiki hii tumemshuhudia Neymar akinaswa kutoka
Santos kwenda Barcelona kwa ada ya Euro 57 milioni, naye Jesuz Navas
alihama kutoka Sevilla kwenda Manchester City kwa Pauni 17 milioni.
Huo ni mwanzo tu, huenda tukashuhudia usajili wa
fedha nyingi zaidi, lakini je ni nani anayeongoza kwa kusajiliwa kwa
fedha nyingi katika historia ya soka? Jibu ni Zlatan Ibrahimovic.
Mchezaji huyo kutoka Sweden ndiye kinara wa fedha
nyingi na amehama kwenye klabu saba tangu mwaka 2002 na kufanya jumla ya
usajili wake kuwa wa Euro 169.1 milioni.
Ibrahimovic alijiunga na PSG akitokea AC Milan
katika dirisha la usajili la msimu uliiopita kwa Euro 23 milioni na hapo
ndipo alitimiza klabu saba tangu alipoanza kuhama.
Mchezaji huyo alianza kwa kuondoka Malmo FF kwenda
Ajax kwa ada ya Euro 9 milioni mwaka 2002, Juventus ililipa Euro 16 kwa
klabu ya Ajax ili kumnasa mwaka 2004, nayo Inter Milan ilimnunua nyota
huyo kutoka Juventus kwa Euro 24.8 milion (2006).
Baadaye Barcelona ilimnunua kwa Euro 69.5 milioni
kutoka Inter Milan (2009). Usajili huo ulishika namba tatu katika
historia ya fedha za usajili duniani.
Mwaka 2011 aliondoka Barcelona kwenda AC Milan kwa
Euro 27 milioni. Lakini Cristiano Ronaldo, aliyehama mara mbili tu
kwenye maisha yake ya soka, anashika nafasi ya tano na amesajiliwa kwa
jumla ya Euro 111.5 milioni.
Mchezaji huyo alitoka Sporting Lisbon kwenda Man
United kisha akaondoka Old Trafford kwenda Real Madrid kwa Euro 94
milioni ukiwa ni usajili mkubwa zaidi kwa mara moja kuwahi kutokea
duniani.
Nyota wa Ireland, Robbie Keane, ndiye mchezaji
ambaye amehama klabu nyingi zaidi tangu mwaka 1999 ambapo ameibuka
kwenye klabu tisa.
No comments:
Post a Comment