Shaffih Dauda
FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi
wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu
mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar
Lenga.
Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari
ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila
mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila
kuondoka nayo.
Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa
habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi
wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo
ndani ya siku saba
Kwa kuipitia barua hiyo bofya: HAPA
Kwa kuipitia barua hiyo bofya: HAPA
No comments:
Post a Comment