Beki
wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akiwania mpira na kipa wa Simba Abel
Dhaira, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara .
Mashabiki wa Simba, walikuwa kama wamemwagiwa maji, wakiwa na huzuni katika kipindi cha kwanza baada ya kufungwa mabao 3-0.
Mshambuliaji Mrisho Ngasa, (kulia) akimtoka beki wa Simba, Joseph Owino, katika kipindi cha pili.
Mshambuliaji
wa Yanga, Didier Kavumbagu (kulia) akiwatoka mabeki wa Simba, Joseph
Owino na Gilbert Kaze, katika kipindi cha kwanza.
Mrisho Ngasa, akiruka kwanja la beki, Gilbert Kaze.
Mashabiki wa Yanga ilikuwa ni furaha kama hivi, ambapo baadaye furaha hii ilizimika ghafla.
Katika
mtanange huo, mashabiki kadhaa walizimia, ambapo shabiki huyu wa Yanga,
akibebwa kutoka jukwaani baada ya kuzimia, huku mashabiki saba wa Simba
na wawili wa Yanga walizimia.
Mshabiki wa Simba walizinduka na kushangweka kama hivi, baada ya kupata bao la pili.
Mrisho Ngasa, akishangilia bao lake la kwanza alilofunga katika dakika ya 15, kipindi cha kwanza.
Mshambuliaji
wa Yanga, Mrisho Ngasa, akishangilia bao lake aliloifungia timu yake
katika kipindi cha kwanza, ambapo bao la pili na la tatu yamefungwa na
Hamis Kiiza.
Wachezaji
wa Yanga, wakishangilia na kumpongeza mwenzao Hamis Kiiza baada ya
kutupia bao la tatu, alilofunga baada ya pasi nzuri kutoka kwa Didier
Kavumbagu.
Hamis Kiiza, akishangilia bao lake la pili, alilofunga kutokana na mpira wa kurushwa na
Mmoja
kati ya mashabiki lukuki waliowasili uwanja wa Taifa kushuhudia
mtanange wa watani wa Jadi Yanga na Simba, akikaguliwa getini kabla ya
kuingia ndani ya uwanja huo, hivi sasa ambapo kila anayeingia
hukaguliwa, huku magari yote yakizuiliwa kuingia na kuruhusiwa magari
maalumu pekee, na kutokana na kuhakiki hilo barabara inayotokea Keko
kuelekea uwanjani eneo ya TCC imefungwa kwa kutumia maroli mawili
makubwa.
Sehemu ya watu wanaoingia uwanjani.....
Beji zikiuzwa kila moja sh. 1000......
Wamiliki wa pikipki hizi wote wamezama uwanjani na kuegesha mashine zao pande hizi za benki ya NBC.
Haya ndiyo marolo yaliyofunga barabara kuzuia magari yasiende Uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment