Raisi
wa Bayern Munich Uli Hoeness, anakabiriwa na kesi ya kukwepa kodi
itakasomwa mwakani, jana alitokwa na machozi wakati akitangaza klabu
yake kuvunja rekodi ya kuingiza mapato makubwa katika cha 113 years.
Katika
mkutano wa mkuu wa klabu, Hoeness, ambaye alipokewa kwa shangwe,
alishindwa kujizuia na kuanza kulia baada ya mabosi wenzie kumsifia
kuiongoza vizuri timu hiyo na kupata mafanikio ya kushinda makombe
matatu msimu uliopita.
Hoeness, ambaye anashtakiwa kwa kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye fedha zake zilizopo katika moja ya benki huko Uswis.
Hoeness,
amekuwa katika klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 40 kama mchezaji, kocha na
saa raisi, alizungumzia matatizo yake ya kisheria, akisema kwamba
alifanya makosa na kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye akaunti yake ya
nje.
'Nilifanya
makosa kutokulipa kodi katika uwekezaji kutoka nje. Sikuchukua
mamilioni ya fedha na kuyatoa nje ya nchi," alisema Hoeness, baada ya
kujifuta machozi. 'Nitapambana na matatizo.'
'Nina imani kubwa na utawala wa kisheria wa Bavarian.
'Ninatumaini
kwamba story hii itakuwa na mwisho mzuri mpaka kufikia mwezi March. Na
kama mpaka wakati huo nitaruhusiwa kuendelea kuwa hapa naahidi
kuitumikia klabu hii mpaka pumzi yangu ya mwisho.'
No comments:
Post a Comment