WENYEJI wa fainali za kombe la Mataifa ya Africa, Afcon 2015, Guinea ya Ikweta wametozwa faini ya dola laki moja kwa mtafaruku wa jana usiku katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ghana ‘Black Stars’.
Hata hivyo CAF imesema Guinea ya Ikweta watahudhuria mechi ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya DR Congo itakayopigwa kesho.
Mashabiki wa timu mwenyeji walifanya vurugu na kuwarushia chupa za maji wachezaji wa Ghana, Viongozi pamoja na mashabiki.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki hao, huku wachezaji wa Ghana wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali.
Vurugu hizo zilisababisha mechi kusimama kwa dakika 35, lakini Ghana walifuzu fainali kutokana na ushindi wa mabao 3-0.
No comments:
Post a Comment