“Kweli mimi si kiongozi wa Simba kwa sasa, lakini
ni mwanachama wa Simba na kikatiba nina haki ya kuendelea kuitumikia
klabu yangu bila kipangamizi chochote hata kuwa Mwenyekiti wa klabu,
haimanishi mimi kujiuzulu ndio mwisho wa kuwa kiongozi katika Simba,
katiba hainizuii hivyo naweza kurudi na kuifanyia kitu klabu yangu kama
kiongozi.”
Kaburu alisema kujiuzulu kwake kama kiongozi ilitokana na kutaka kupumzika na kujipanga upya.
“Watu wasiwe na hofu, ninakuja upya na wakati huu
nitaangalia matatizo mbalimbali na kuyasuluhisha ili klabu kama klabu
ifanikiwe,”alisema.
“Sasa nimetoka kwenye uongozi, nafikiri bado mimi
mwanachama wa Simba naruhusiwa kutoa maoni yangu au hata saa zingine
kuisaidia Simba kwenye mambo mbalimbali,” alisema Kaburu, ambaye
kuonekana kwake mazoezi katika siku za karibuni kuliibua mjadala kwa
mashabiki.
No comments:
Post a Comment